Usichokijua kuhusu WhatsApp Business kwa ajili ya Wajasiriamali wadogo.

Kipindi kichache kilichopita WhatsApp ilizindua Programu yao mpya ya WhatsApp Business inayowawezesha wafanya Biashara wadogo wadogo kuweza kuendesha Biashara zao kupitia mtandao huo wa WhatsApp. Leo nimekuletea  Baadhi ya vipengele vipya ambavyo havipatikani kwa mtumiaji wa whatsapp ya kawaida;

Kuacha Ujumbe Pale unapokuwa uko mbali na Simu.

Japo sio kitu kipya katika mitandao ya kijamii ikiwepo Facebook Messenger ndio ilianzisha huduma hiyo ya kuacha ujumbe mfupi (Welcome Message). Kipengele hiki kinaweza kukufanya uweze kuset aina ya ujumbe unaotaka umfikie mteja wako pale anapokutumia ujumbe na kuweza kumjibu papo hapo utakapokuwa uko mbali na simu yako.

Usikose Kusoma:  Windows phone 8 vs android niende wapi?

Wasifu wa Biashara

Kwa kutumia WhatsApp Business utaweza kuweka wasifu wa biashara yako na maelezo mengine ya Biashara inapopatikana na kazi unazozifanya na website ya biashara yako

Kudhibiti Miamala

Whatsapp Business inakuwezesha kudhibiti miamala ya wateja wako kwa kutambua mteja mpya, mteja aliyelipa na mteja ambaye bado hajalipa katika biashara hiyo.

Usikose Kusoma:  Chromebook Pixel: Laptop ya kisasa ya google yazinduliwa

Kwa sasa Programu ya Whatsapp Business inapatikana kwa simu za Android tu unaweza ipakuwa hapa

Tufuatilie kwenye mitandao mbali mbali ili usipitwe na Habari, Uchambuzi naMakala mbali mbali ya mitanadoni na ya kiteknolojia kwenye FacebookTwitterInstagram, Google+ na Youtube, Pia usisite kutoa maoni yako hapo chini au tuandikie barua pepe kwa mhariri@mtaawasaba.com

3 MAONI

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa