Apple waachia iOS 11.2.6 kutatua tatizo linaloharibu iPhone

Mwandishi Alexander Nkwabi
Apple waachia iOS 11.2.6 kutatua tatizo linaloharibu iPhone. Mapema mwezi huu kumetokea tatizo kubwa lililokumba simu za iPhone. Neno la kihindi (Telugu) ambalo likiandikwa kwa kutumia app kama iMassage, WhatsApp, Pamoja na FB Messenger lilisababisha kukwama na kushindwa kufanya kazi kabisa.

telugu-bug-800x673

 

Tatizo hili limegundulikwa juma lililopita ambapo mtu yoyote aliyetuma neno hilo lilisababisha simu kukwama na hata kumzuia mtumiaji kutumia app za kutuma ujumbe. Tatizo hili limeathiri pia kisakuzi cha Safari na app zingine zenye huduma ya kutuma ujumbe kwenye macOS na Apple watch.

Leo Apple wameachia iOS 11.2.6, kama sasisho la mfumo endeshi iOS 11. Kati ya maboresho yaliyokuja na sasisho hili, ni pamoja na kutatua tatizo hili ambalo limezikumba simu za iPhone.

update

Na kwa kuwa tatizo hili limekumba pia kisakuzi cha Safari na app zingine zenye huduma ya kutuma ujumbe kwenye macOS na Apple watch, Apple wameamua kuachia sasisho kama hili kwa mifumo endeshi mingine ikiwemo watchOS, tvOS, na macOS ili kuzuia tatizo hili kujitokeza tena.

Utatuzi wa tatizo hili haujaangalia lughaa ya kihndi (telugu) pekee, bali imezingatia kurekebisha hata kwenye lugha zingine.

Endelea kuwa nasi kwa kutufuata kwenye mitandao ya kijamii, na usisahau ku subscribu ili uwe wa kwanza kupata Habari, Uchambuzi na Makala mbali mbali za kisayansi na teknolojia. Pia usisahau ku acha maoni yako hapo chini na unaweza kuwasiliana nasi kwa barua pepe mhariri@mtaawasaba.com

 

 

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive