Apple wazindua iPad mpya ya gharama nafuu yenye kusupport Apple pencil

Baada majuma kadhaa ya tetesi kuhusu Apple kuachia iPad mpya, leo Apple wamezindua rasmi tableti waliyoiita”iPad ya gharama nafuu kuliko zote” na itakuwa na uwezo wa kufanya kazi na kifaa cha Apple pencil. Uzinduzi huu ambao ulikuwa umekaa kielimu elimu zaidi ulifanyika katika shule ya Lane Tech College Prep High School huko jijini Chicago, Marekani.

iPad-9-7-inch-Apple-Pencil-support_32718

Tableti hii mpya iliyozinduliwa leo, itaanza kuuzwa kwa bei ya dola za kimarekani 299 kwa ajili ya mashule, na wanafunzi watapata hifadhi ya bure ya iCloud yenye kufikia GB 200 tofauti na watumiaji wa kawaida ambao watapata GB 5 pekee. Pia wanafunzi wataweza kununua Apple pencil kwa bei iliyoshushwa ya dola za kimarekani 89.

DSCF7379_2500_resized

Sifa zake

iPad hii mpya inafanana sana na ile yenye inchi 9.7, ila hii ina support Apple pencil. ina rangi za silver, space gray na rangi ya dhahabu ambayo ni mpya. Betri yake ina uwezo wa kukaa na chaji mpaka masaa 10, tableti hii ina kioo chenye Retina Display, inakuja na chip ya A10 Fusion na pia ina hifadhi ya GB 32 na uzito wa paundi moja.

iPad-9-7-inch-AR-sensors_32718

Bei na upatikanaji

  • itaanza kuuzwa kwa dola za kimarekani 329 kwa iPad zenye GB 32 na Wi-Fi, huku zile ambazo zina Wi-Fi na uwezo wa kuweka laini ya simu zitauzwa kwa dola za kimarekani 459
  • Apple pencil inaanza kuuzwa kwa bei ya dola za kimarekani 99 na inauzwa peke yake. Kwa mashule watanunua iPad kwa dola za kimarekani 299 na Apple pencil kwa dola za kimarekani 89

Ahsante kwa kufuatilia kwa kina makala hii, Pia usisiste kutoa maoni yako hapo chini, Pia usisahau kuSubscribe katika Chanel yetu ya Youtube  uweze kupata video za kila wiki kupitia youtube. Kwenye mitandao ya kijamii instagram, twitter na facebook tufuate @Mtaawasaba

WAWEZA SOMA:  Robot huyu ana uwezo wa kutambua watu na kucheza muziki

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa