Apple wazindua iPhone 13 Pro na Pro Max zikiwa na kioo chenye 120Hz

Mwandishi Alexander Nkwabi
Apple wazindua iPhone 13 Pro na iPhone 13 Pro Max zikiwa zinapokea kijiti kutoka kwa watangulizi wake iPhone 12 Pro na iPhone Pro Max. Uzinduzi huu umetangazwa kwenye Apple event siku ya jumanne tarehe 14, 2021, pamoja na simu hizi pia Apple wamezindua iPhone 13 na iPhone 13 Mini.

Simu hizi mbili zinaingia sokoni zikiuzwa kwa bei sawa na ya watangulizi wake, ambapo  iPhone 13 Pro itauzwa kwa dola za marekani 999 sawa na shilingi za tanzania milioni 2 na laki 3 huku iPhone 13 Pro Max ikiuzwa dola za kimarekani 1,099 sawa na milioni 2 na laki 6, bei hizi zinaweza badilika kutokana na kupanda au kushuka kwa shilingi ya Tanzania.

Kama kawaida yao Apple, tofauti kati ya simu za pro na zilizobaki ni kamera, hata iPhone 13 Pro haziko tofauti na watangulizi wake. Zinakuja kamera tatu au kama tunavoziita wenyewe macho matatu zikiwa na lenzi ya telefoto yenye ukubwa wa milimita 77 yenye uwezo wa ku zoom x3 tofauti na mtangulizi wake ambapo iphone 12 pro ilikuwa na uwezo wa kuzoom x2.5

Pia inakuja na kipengele kipya kwa jina la ProMotion ambacho kwa mara ya kwanza kabisa kinakuja kwenye simu za iPhone, huu ni mpangilio unaofanya simu iwe nyepesi na laini kuitumia, kipengele hiki kipo kwenye simu za android kama Samsung na zingine maarufu kama 120Hz refresh rate.

Habari hii bado inaboreshwa

 

Avatar of alexander nkwabi
Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive