Bakhresa kuja na Azam Telecom

Akizungumza na gazeti la kila siku la The Citizen,  Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa kampuni ya Bakhresa Group, bwana Hussein Sufian Ally amesema kundi la makampuni ya Bakhresa linazidi kupanua wigo wake na kuingia katika uwanja wa mawasiliano.

Ndani ya miezi michache ijayo wanatarajia kuzindua mtandao wa Azam mobile kwa nchi nzima ya Tanzania.

Kampuni hiyo ambayo itakuwa kama sehemu ya kundi la makampuni ya Bakhresa chini ya umiliki wa Said Salim Bakhresa, itajulikana kama Azam Telecom (T) limited,

Akizungumza bwana Ally amesema mtandao huu unalenga kuleta huduma nzuri lakini kwa gharama nafuu kwa wanachi wa Tanzania. Tayari wameshapata vibali kutoka TCRA vitakavyowezesha wao kutoa huduma za mawasiliano ikiwemo huduma ya intaneti ya kasi ya 4G

Usikose Kusoma:  Laini za simu za TTCL zinatolewa bure

Pia watatoa huduma zingine nyingi katika wanja wa mawasiliano,

Endelea kutembelea Mtaawasaba ili tuendelee kukupa undani wa taarifa hii. Pia usisahau ku subscribe kwenye mitandao yetu ya kijamii @Mtaawasaba na pia YouTube channel yetu ya Mtaawasaba

Leave a Reply