Bitcoin: Yote unayohitaji kufahamu

Mwandishi Alexander Nkwabi

Bitcoin ni mfumo wa kidigitali wa malipo kwenye mtandao wa internet (cryptocurrency), Imekuwepo tangu mwaka 2009. Mfumo huu ulitengenezwa na programa/maprograma anae/wanao julikana kwa jina la Satoshi Nakamoto. Mpaka leo hakuna mtu au kundi aliyethibitisha/lililothibitisha kuwa ndio Satoshi Nakamoto. Unaweza kutumia Bitcoin kununua vitu mbalimbali kama ilivyo kwa hela za karatasi, hata hivyo fedha hii inatofautiana na fedha ya karatasi kwa namna nyingi.

Bitcoin zinatengenezwaje? Thamani yake inapatikanaje? Zina faida gani? Je, hasara zake ni zipi? Kuna maswali mengi kuhusiana na Bitcoin. Endelea kusoma makala hii upate mwanga wa kuijua Bitcoin kiundani. Ili kuielewa Bitcoin lazima kwanza tujue cryptocurrency ni nini?

Unaweza kusoma: Cryptocurrency ni nini?

Bitcoin ni aina ya fedha ya kielektronikii inayoweza kutumika kufanyia manunuzi mtandaoni. Zinapokelewa na makampuni makubwa kwa madogo ikiwemo Microsoft. Kwa sababu ya thamani kubwa ya fedha hii, unaweza kugawanya moja kwa desimali nane, maana yake unaweza kutuma mpaka Bitcoin 0.00000001.

Bitcoin mtaawasaba

Kinachoifanya Bitcoin na fedha zingine za kimtandao kuwa tofauti ni kuwa hakuna anaezisimamia kama ilivo kwa benki ama serikali bali zinafatiliwa na mfumo wa kompyuta usio usiosimamiwa na mtu au kikundi cha watu. Zinatumwa kupitia kompyuta au kifaa cha mkononi, ambapo kila muamala uwa unawekwa kumbukumbu kitu kinachoitwa blockchain

  • Blockchain ni nini? [tutaona hii kwenye makala ingine]

Bitcoin zinahifadhiwa kwenye pochi za kidijitali “digital wallet” ambazo zinaweza kuwa kwenye kompyuta yako au hewani. Njia zote zina faida zake na mapungufu yake.

Zinapatikanaje?

Icarus_bitcoin_mining_rig-1024x768-1-768x576

Kama tulivoona kwenye makala ya cryptocurrency, basi Bitcoin nazo zina njia mbili ya kuzipata. Njia ya kwanza ni ya uvunaji [mining] ambayo watu duniani kote hushindana kujibu maswali magumu sana ya kimahesabu na mshindi uwa anapata kipande cha Bitcoin zitakazokuwa zimetengenezwa.

Unaweza dhani ni mchakato mrahisi, la hasha. Ili uweze kuvuna unahitaji vifaa mahususi kwa ajili ya kazi ya uvunaji ambavyo hufanya kazi muda wote kutwa kucha.

Uvunaji hautawezekana tena zitakapokuwa zimetengenezwa Bitcoin millioni 21

Mchakato wa uvunaji umetengenezwa kusimama wenyewe, na uvunaji hautawezekana tena zitakapokuwa zimetengenezwa Bitcoin millioni 21. Jambo hilo litatokea mwaka 2140.

Kama hauna vifaa vya kufanyia kazi ya uvunaji usikate tamaa, bado unayo fursa ingine, ambayo ni kununua Bitcoin kupitia mawakala mbalimbali wanaouza na kununua Bitcoin kwa fedha ya eneo lako. Mfano unaweza kutembelea Localbitcoins uweze kununua au kuuza Bitcoin kwa fedha ya eneo lako.

Thamani ya Bitcoin?

Cryptocurrencies-4

Hata ivyo thamani ya Bitcoin inaweza kupanda sana au kushuka sana kupita kiasi ndani ya siku moja.

 

Faida na hasara za Bitcoin

Cryptocurrencies-2

Faida namba moja ni usiri wa taarifa za miamala, hakuna taarifa binafsi ambazo zitajulikana kuhusu mtoaji au mpokeaji. Na hii imekuwa changamoto kwa mataifa mengi kuukubali mfumo huu maana ni mfumo salama kwa makundi ya kihalifu.

Lakini pia faida ingine ni kuwa hakuna Bitcoin feki, zote ni halali, tofauti na fedha za karatasi ambazo zinaweza kughshiwa.

Usalama wa Bitcoin ni changamoto bado, kama ikitokea mtaalamu wa kompyuta aka hack digital wallet yako basi unaweza poteza utajiri wako wote au kama umeweka offline na hard drive ikaibiwa au ikaharibika basi utakuwa umepoteza kila kitu.

Miamala ya Bitcoin uwa hairudishwi, kama umekosea wakati wa kutuma, au kama ulichotaka kununua sicho au kwa namna yoyote haitawezekana kurudishiwa sarafu zako pale unapofanya muamala.

Mfumo huu bado ni mchanga, unakua kwa kasi na mambo mengi yanaweza kutokea hapo katikati. Thamani inaweza kupanda ghafla kwa kasi ya ajabu au ikashuka kw akiasi ambacho si cha kawaida. Hivo inashauriwa usiwekeze kwenye Bitcoin kiasi kikubwa cha fedha ambayo hauko tayari kuipoteza.

Mbadala wa Bitcoin

Cryptocurrencies

Kuna sarafi zingine za kimtandao nyingi zinazopatikana, ambazo zinafanya kazi kama Bitcoin, kuna karibu sarafu tofauti tofauti 1000. Hizi ni rahisi kuvuna lakini sio sehemu nyingi zinapokelewa au zinatumika kama Bitcoin na zinaweza kupoteza thamani yake kwa haraka

Baadhi ya  sarafu zingine za kimtandao ambazo zinaweza kuwa mbadala wa Bitcoin ni  kama Safecoin,  Ethereum, Litecoin, Dash, Ripple, na Monero, kwa uchache wao.

Neno la mwisho

Maoni yako ni yapi kuhusu Bitcoin? Ushawahi kuzitumia? Tuandikie kwenye maoni hapo chini. Na hayo ni baadhi ya mambo ambayo nimekuandalia leo kuhusu Bitcoin, naamini umepata mwanga sasa, ili kujua zaidi kuhusu Bitcoin endelea kutembelea Mtaawasaba.

Avatar of alexander nkwabi
Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive