Cryptocurrency sio neno geni masikioni kwako ndugu msomaji. Ni mada ambayo imekuwa ikizungumziwa sana hasa hasa kipindi cha miaka ya hivi karibuni. Lakini je, tunajua cryptocurrency nini? inafanyaje kazi? inapatikanaje? Ungana nami katika makala hii tukiangazia yote kuhusu cryptocurrency.
Inawezekana ushawahi kusikia neno cryptocurrency siku zilizopita. Lakini unajua nini kuhusu neno hilo? Cryptocurrency ni nini haswa? Neno hili limeleta mkanganyiko mkubwa kwa wengi hasa kwenye dunia ya kidijitali.
Twende pamoja ili tuweze kuondoa baadhi ya mkanganyiko huu, tumeandaa maelezo ambayo yatakupa mwangaza kuhusiana nayo, inaptikanaje, inafanyaje kazi? faida zake na kadhalika.
Cryptocurrency ni nini haswa?
Kwa maelezo rahisi kabisa Crypocurrency ni mfumo wa kifedha wa kidijitali unaokuruhusu kununua vitu mtandaoni. Ni kama hela hizi za kawaida isipokuwa hizi ni mtandaoni tu, tofauti ya fedha hizi na zile tulizozizoea ni kuwa Cryptocurrency hazisimamiwi wala kumilikiwa na Serikali au benki. Hii ina faida zake na hasara zake ambazo tutazichambua huko chini.
Cryptocurrency au hela ya kimtandao unayomiliki inahifadhiwa kwenye “digital wallet” au kwenye kompyuta iliyo offline au kwenye simu janja yako. Kila muamala wa Cryptocurrency unarekodiwa kwenye blockchain ambapo uko wazi kwa watumiaji wote kuuona.
Uvunaji (mining) ni nini?
Sasa tumeshajua Cryptocurrency ni nini? Swali linalofuata ni inapatikanaje? Cryptocurrencies zinapatikana kwa kuvunwa (mining). Uvunaji huo hufanywa kupitia kompyuta, ambayo hujaribu kufanya mahesabu makubwa na magumu yanayoitwa hash.
Watu dunia nzima wanashindana kuvuna na atakaekuwa mshindi anapata sehemu ya cryptocurrency aliyovuna. Mchakato huu wa uvunaji unahitaji mashine(komyuta) maalumu zinazofanya kazi kutwa kucha.
Uvunaji sio njia pekee ya kupata cryptocurrencies, Njia rahisi ni kununua kupitia wauzaji mbalimbali walioko kwenye masoko ya kuuza na kununua cryptocurrency.
Bitcoin ndio cryptocurrency yenye bei ghali kuliko zote, inauzwa mpaka mpaka shilingi za kitanzania millioni 50 (wakati mada hii ikiandikwa). Na bei yake imekuwa ikipanda na kushuka sana.
Unaweza kufanya nini na cryptocurrency?
Kununua vitu
Zamani ilikuwa ngumu kupata wauzaji wanaokubali kupokea Crypocurrencies kama njia ya malipo. Siku izi imekuwa jambo la kawaida kuona watu mbalimbali wakipokea cryptocurrency.
Kuwekeza
Mwanzoni watu walinunua cryptocurrencies kwa gharama ndogo sana kisha wakaziacha tu. Mara ghafla miaka ya hivi karibuni watu wamekuwa mamilionea kwa fedha zao walizohifadhi miaka iyo na kuzisahau. Mfano Bitcoin ambayo ilikuwa na thamani ya dola za kimarekani 800 kwa bitcoin moja, mwezi wa 11, 2017 ikapanda ghafla na kufikia dola za kimarekani 7000 kwa kila bitcoin.
Uhalali wa cryptocurrencies
Kadri umaarufu wa cryptocurrencies unavozidi ndio vyombo vya sheria na mamlaka za kodi vinajaribu kuelewa namna hizi cryptocurrencies zinavofanya kazi na namna ya kuziingiza kwenye utaratibu wa kila siku wa uhalali kisheria.
Kufikia novemba 2017, matumizi ya Bitcoin na sarafu zingine za kimtandao zimepigwa marufuku kutumika kwenye nchi kama Bangladesh, Bolivia, Ecuador, Kyrgyzstan na Vietnam, na siku za hivi karibuni China na Urusi wamezizuia kutumika katika nchi hizo. Ili kusema mfumo huu ni halali au sio halali inategemeana na sheria za nchi husika.
Faida na hasara ya cryptocurrencies
Moja ya faida kubwa ya mfumo huu ni kutojulikana taarifa za mnunuaji au muuzaji. Japo taarifa za miamala kuwekwa wazi watu wote waone, hakuna taarifa binafsi zinazooneshwa kama jina au anwani ya muuzaji au mnunuaji
Cryptocurrencies ni maarufu kwa makundi ya kihalifu maana ni ngumu kujulikana
Ni faida na hasara kwa wakati mmoja. Cryptocurrencies ni maarufu kwa makundi ya kihalifu maana ni ngumu kujulikana. Hii ndio sababu kubwa serikali nyingi duniani zinazua matumizi ya Cryptocurrencies au zinajaribu kutengeneza mazingira ya uwazi wakati wa kununua au kuuza kwa kutumia mfumo huu.
Kutumia njia hii ya Cryptocurrencies kufanya biashara ni njia nzuri na rahisi japo kuna gharama ndogondogo ambazo unatakiwa ilipe kwa kila muamala unaofanyika ambao ni ndogo ukilinganisha na gharama zainazotozwa na mabenki.
Faida moja kubwa kuhusu Cryptocurrencies ni kuwa haiwezi kughushiwa, yani hakuna Cryptocurrency feki kama ambavyo hela za kawaida inavowezekana.
Usalama wa mfumo huu nao umekuwa ni moja ya changamoto kubwa. Kama tulivosema hapo mwanzo hizi hela zinahifadhiwa kwenye digital wallet ambapo mtu akifanikiwa kuhack anaweza kukuibia. na kwa wale wanaohifadhi kwenye kompyuta zao zilizo offline ikitokea hard disk ikafa au kuibiwa basi unakuwa umepoteza utajiri wako wote.
Changamoto iliyokubwa kuliko zote ni kwamba miamala inayofanyika kwa Cryptocurrencies uwa hairudishwi. Ikitokea unafanya biashara na mtu tapeli au kama hukuridhika na bidhaa uliyonunua basi hela yako inakuwa imeenda jumla. Tofauti na kutumia credit card hela yako inaweza kurudishwa iwapo haujaridhika na ulichokilipia na ukaamua kurudisha.
Cryptocurrencies kubwa unazotakiwa kuzijua
Bitcoin ndio kubwa kuliko zote na ndio maarufu zaidi duniani ikiwa na watumiaji mamilioni dunia nzima. Ilianzishwa na mtu au kikundi cha watu anaejiita Satoshi Nakamoto mwaka 2009. Kwa sasa kuna Cryptocurrencies tofauti tofauti zaidi ya 1000
Pamoja na kuwepo idadi kubwa, utagundua kwamba zinazotajwa sana ni zile kubwa kubwa zenye majina. Ambazo ni kama Ethereum (ETH) , Bitcoin Cash (BCH) , Ripple (XRP) , Dash (DASH), Litecoin (LTC) , Ethereum Classic (ETC) na zingine nyingi. kwa mujibu wa taarifa kutoka CoinMarketCap.
Mijadala ya cryptocurrencies?
Tembelea link hizi hapa chini uweze kujisomea mambo mbalimbali kuhusu crypocurrencies.
- CryptoCompare
- Cryptocurrency Talk
- Bitcoin Talk
- Coingage
- Bitcoin Wealth Club
- BTC Warriors
- Bitcoin Subreddit
- Ethereum Subreddit
- Litecoin Subreddit
- Cryptocurrency Subreddit
Neno la mwisho
Tumeshaona sasa Cryptocurrency ni nini, inapatikanaje, inafanyaje kazi, hasara zake na faida zake. Mfumo huu wa manunuzi haushi leo japo sarafu ndogo ndogo zinaweza zikapotea ila kubwa kubwa kama bitcoin na Ethereum zitaendelea kuwepo kwa muda mrefu tu
Thamani ya Cryptocurrencies inaweza kupanda au kushuka kwa kiasi kikubwa cha dola kwa siku moja. Inashauriwa usitumie kiasi kibwa kuwekeza kwenye Cryptocurrencies ambacho hauko tayari kukipoteza
Ushawahi kutumia cryptocurrencies? Ipi? Tuandikie kwenye maoni yako.