[DEAL] Tigo kwa kushirikiana na Samsung, Infinix, na Tecno waja na wiki ya simu janja kupitia duka la Jumia

Akitangaza ushirikiano huo kabambe jijini Dar es Salaam, Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema kuwa Mobile Week itakayoanza 24 – 30 Machi wateja wataweza  kununua simu za kisasa na kwa bei nafuu zaidi ambazo hazijawahi kutokea nchini, huku kila simu ikiwa na ofa ya hadi GB 18 za intaneti kutoka Tigo.

Hata hivyo Jumia tayari imeshaanza kutoa ofer hiyo tarehe 18 machi 2018, huku tigo ikisema itaanza kutoa ofa hiyo kuanzia machi 24. Unaweza tazama ofa hizi kupitia Hapa www.jumia.co.tz Pamoja na hayo pia kuna mashindano ya kupata vocha ya papo pa kwapo ambayo mteja ataweza jishindia vocha kuanzia shilingi ,5000 hadi 10,000.

‘Tigo inaongoza katika mageuzi ya maisha ya kidigitali. Lengo letu ni kuongeza idadi ya watumiaji wa simu za kisasa nchini huku tukihakikisha kuwa wateja wetu wote wanapata huduma bora, za uhakika za mtandao. Huduma bora za kidigitali zinaanza na vifaa  bora, ndio maana ushirikiano wetu na Jumia utahakikisha kuwa kila mmoja anapata simu mpya ya kisasa pamoja na ofa za intaneti zitakazomwezesha mtumiaji kuwa sehemu ya maisha ya kidigitali,’ alisema.

Akifafanua jinsi ya kupata ofa hizi za simu, Mkurugenzi Mtendaji wa Jumia Tanzania, Zadok Prescott aliwashauri wateja kutembelea tovuti ya www.jumia.co.tz ambapo watapata aina mbali mbali za simu kutoka kwa wauzaji mbali mbali. Baada ya hapo wanaweza kuchagua aina ya simu wanayoipenda na kutoa maelekezo ya sehemu ambapo wangependa kuletewa simu yenyewe na watoa huduma wa Jumia. Wasiokuwa na huduma za mtandao wanaweza kupiga simu namba 0800 710024 bila gharama yoyote ili kutoa maombi ya simu wanayoitaka.

WAWEZA SOMA:  Apple kununua app ya kutambua muziki ya Shazam

‘Nawahamasisha nyote mchangamkie ofa kabambe za simu zitakazopatikana katika mtandao wa Jumia katika kipindi hiki cha Mobile Week. Tunafurahia kuleta pamoja baadhi ya kampuni kubwa zaidi za simu duniani kama vile Tigo,  Samsung, Tecno na Infinix kushiriki katika gulio hili la kila mwaka. Kwa pamoja tumefanikiwa kuwaletea ofa ambazo hazijawahi kutokea kwa simu za kisasa, ikiwemo simu zenye uwezo wa 3G zitakazopatikana kuanzia TZS 50,000/- pekee na zile za 4G zitakazopatikana kwa chini ya TZS 150,000/- tu,’ Zadok alisema.

Wateja watafurahia punguzo kubwa la bei hadi 60% kwa simu za kisasa (smartphone) kupitia Jumia Mobile Week (wiki ya simu) itakayofanyika kwenye mtandao wa manunuzi ya bidhaa wa Jumia (www.jumia.co.tz). Pamoja na punguzo hili kubwa la bei, simu zote za kisasa zitakazouzwa katika promosheni hii zitakuwa na ofa ya hadi GB 18 ya intaneti bure kutoka kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ya Tigo Tanzania.

‘Wateja wana uhuru wa kuja kuchukua simu zao kutoka katika ofisi za Jumia ama wanaweza kuletewa simu zao mahali popote walipo. Malipo kwa ajili ya simu yatafanyika kwa njia ya Tigo Pesa au kwa pesa taslim mara tu baada ya mteja kupokea simu aliyoagiza na sio vinginevyo. Hii inaondoa hofu ya  kutapeliwa,’ Zadok alimaliza.

Ukuaji wa simu za kisasa (smartphone) unatoa fursa kubwa kwa matumizi ya mtandao kutoa huduma mbali mbali kwa Watanzania kupitia mifumo kama Jumia. Hivi karibuni idadi ya watumiaji wa simu za mkononi nchini ilifikia watu milioni 40, huku idadi ya wanaotumia mtandao ifikia watu 23 milioni.

Katika uzinduzi wa gulio hilo la simu kwa njia ya mtandao, Jumia pia walizindua Ripoti ya Sekta ya Simu za Mkononi Tanzania inayoonesha kuwa asilimia 83% ya Watanzania walitembelea mtandao wa Jumia kupitia simu zao za mkononi, ikilinganishwa na asilimia 17% tu waliotumia kompyuta. Matokeo haya yanadhihirisha kuwa Watanzania wengi wamevuka kigezo cha matumizi ya kompyuta na badala yake wanatumia teknologia ya  simu za mkononi kutekeleza shughuli zao za kila siku.

WAWEZA SOMA:  Kashfa ya Cambridge Analytica yafanya Facebook kuzindua programu kusafisha mipangilio yako ya faragha.

“Idadi ya watu wanaotumia simu za kisasa inakua kwa kasi siku hadi siku. Hii ni hatua muhimu katika maendeleo ya simu za mkononi, ila upatikanaji wa vifaa vya kisasa bado ni changamoto kubwa. Jumia imejikita kuhakikisha kuwa Watanzania wote wanapata simu za kisasa, hasa katika kipindi hiki cha Mobile Week,” Zadok alibainisha.

 

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa