Facebook kuunganisha WhatsApp, Facebook Messenger na Instagram

Facebook ina mpango wa kuunganisha huduma za kutumiana jumbe za WhatsApp, Instagram na Facebook Messenger. Japo app zote tatu zitakuwa zikifanya kazi kwa kujitegemea, mfumo wa kutuma jumbe utaunganishwa, hii ina maana kwamba, mtumiaji wa whatsapp atakuwa na uwezo wa kumuandikia mtumiaji wa Instagram moja kwa moja, ambapo kwa sasa haiwezekani.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika vilivowasiliana na jarida la New York Times  vinasema muunganiko huu utakamilika mwishoni mwa mwaka 2019 au mwanzo wa 2020.

Muunganiko huu utawezesha huduma zote kutumia mfumo wa ulinzi wa end-to-end encryption wakati wa kutuma na kupokea jumbe, mfumo huu ambao kwa sasa unapatikana kwa watumiaji wa WhatsApp pekee utawezesha kuboresha faragha ya jumbe zinazotumwa hasa kutoka Facebook Messenger na Instagram DM.

Mpaka sasa haijajulikana sababu kubwa ya kuunganisha huduma hizi tatu, ila inasemekana ni kwa ajili ya kuvutia makampuni kutangaza na washirika zaidi. Instagram ambayo inajinadi kuwa na watumiaji hai zaidi ya bilioni 1 kwa mwezi huku WhatsApp ikidai ina watumiaji hai zaidi ya bilioni 1.5, kwa kuunganisha watumiaji wote kwa pamoja Facebook inakuwa na wigo mkubwa wa kuwafikia walengwa wa matangazo husika.

Mkurugenzi mtendaji wa Facebook Mark Zuckerberg ndio anaesemakana yuko nyuma ya mkakati huu wa kuunganisha huduma hizi tatu, na hii ilikuja muda mfupi tu baada ya Facebook kununua Instagram na WhatsApp. Waanzilishi halisi wa Instagram na WhatsApp kwa nyakati tofauti waliamua kuacha kufanya kazi kwenye makampuni hayo baada ya Facebook kuanza kutumia taarifa za watumiaji wake kupata faida.

WAWEZA SOMA:  Wireless Storage: Njia rahisi ya kuhamisha Data kwenye simu yako ya android.

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa