Apple kuhamia kwenye vioo vya OLED kwa iPhone zote kuanzia 2019

Kuna ripoti ambazo zimeanza kuenea kuwa kampuni ya simu ya Apple itaanza kutumia vioo vye teknolojia ya OLED kwenye modeli za simu zake zote za iPhone kuanzia mwaka 2019.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Electronic Times ya Korea kusini inasema Apple wataacha kabisa kutumia vioo vyenye teknolojia ya LCD kwa iPhone zote zinazotoka mwakani.

Kwa sasa simu pekee ya Apple inayotumia kioo chenye teknolojia ya OLED ni iPhone X ambayo ilitoka mwishoni mwaka 2017. Na kukaanza kuwa na taarifa za Apple kuanza kuhama taratibu kutoka kwa teknolojia ya LCD kwenda OLED kwa simu zitakazoanza kutoka 2019.

Usikose Kusoma:  Zuckerberg achapisha ukurasa mzima kwenye gazeti kuomba radhi juu ya kashfa ya Cambridge Analytica

Kwa mujibu wa tovuti hiyo ya korea kusini, habari hii sio njema sana kwa makampuni wasambazaji wa vioo vyenye teknolojia ya LCD kwa Apple, hisa za kampuni ya Japan Display ambao ndio wasambazaji wakuu wa vioo vya LCD kwa Apple zimeshuka kwa asilimia 10 na kwa kipindi kimoja zimeshuka mpaka asilimia 21, kwa mujibu wa ripoti kutoka shirika la habari la Reuters, kampuni hiyo imeanza kutengeneza vioo vyenye teknolojia ya OLED na inatafuta wafadhili kwa mradi huo.

Makampuni mengine ambayo pia ni wasambazaji wa vioo hivyo hayakuachwa salama ikiwemo kampuni ya Sharp, ambayo hisa zake zimeshuka kwa asilimia nne kufuatia habari hii.

Usikose Kusoma:  Vita ya simu zinazokunjika: Hii ndiyo Huawei Mate X

Sababu kubwa ya Apple kuhamia kwenye teknolojia hii ni kwenda na kasi ya soko ambayo kwa sasa Samsung ndio yuko mbele kwa kutumia teknolojia hiyo kwa simu zake zote ambazo ni flagship. Samsung Display Co, ambayo ni kampuni inayotengeneza vioo vya OLED ndio wasambazaji wakuu wa vioo hivyo kwa Apple pia ndio wasambazaji kwa kampuni dada ya Samsung Electronics,  hivyo kufanya mahitaji kuwa makubwa. Kampuni ingine ya LG Electronics pia inatengeneza vioo vya OLED ila sio kwa ubora na idadi kama ya Samsung.

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa