FIFA waruhusu teknolojia ya video (VAR) kutumika kwenye Kombe la dunia 2018

Kwa mara ya kwanza kabisa

Teknolojia ya video katika mchezo wa soka au kama inavojulikana kama Video assistant referees (VAR) inatarajiwa kutumika katika michano ya kombe la dunia litakalopigwa siku zijazo mwaka huu 2018 huko Urusi. Hii ni baada ya watunga sheria za mchezo huo kuafikiana kuhusu kuanza kutumika kwa teknolojia hiyo.

Bodi ya shirikisho la michezo la kimataifa (Ifab) lilipitisha matumizi bila mjumbe hata mmoja kupinga kwenye mkutano huko Zurich. Na huo ndio unakuwa mwanzo wa matumizi ya teknolojia hii moja kwa moja.

Usikose Kusoma:  TTCL kutumia mabilioni kusambaza huduma ya internet majumbani

Akithibitisha habari hii, Rais wa Shirikisho la soka Duniani(FIFA), Gianni Infantino amesema kuwa tunahitaji kuishi kulingana na wakati, ni lazima tuwapatie waamuzi wetu vifaa vyenye ubora ambavyo wataweza kufanya kazi kwa urahisi na kutoa maamuzi yaliyo sahihi na katika kombe la dunia hayo maamuzi yanahitajika.

Teknolojia hii ya video kwenye mchezo wa soka tayari imekuwa ikifanyiwa majaribio katika michezo ya ligi za ndani za nchini Uingereza na pia liki za Ujerumani pia Italia kabla haijaruhusiwa rasmi.

Usikose Kusoma:  Ifahamu simu ya Samsung Galaxy Note 8

teknolojia ya VAR itatumika kama njia ya kupunguza makosa ambayo ni ya wazi kabisa ambayo refarii anaweza asiyaone wakati mechi inaendelea.

Baadhi ya mambo ambayo teknolojia hii itakuwa ikiangalia ni kama: Goli limeingia au la, Penati ni ya halali au la, Mtu apewe kadi nyekundu ya moja kwa moja au la, kukosea mtu (pale refarii anapomtoa mtu ambae hausiki na kumuacha mwenye makosa)

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa