Instagram yazindua IGTV, programu tumishi kwa ajili ya video ndefu.

IGTV ni jaribio la Instagram kuanzisha mfumo wa kurusha Video ndefu kama YouTube, ambapo hapo awali Instagram ilikuwa ikiruhusu watumiaji kupakia mpaka video za dakika moja pekee, lakini hayo yamebadilika kuanzia leo kwani kupitia IGTV watumiaji wataweza kupakia mpaka video zenye urefu wa saa nzima.

Kutakuwa na channel maalum kwa ajili ya kurusha video ndefu na mtumiaji ataweza kuona kupitia toleo jipya la instagram ambalo tayari limeshaanz akupatikana na pia kupitia programu tumishi ya IGTV ambayo tayari imeshaanz akupatikana kwenye Android na iOS.

Usikose Kusoma:  Facebook kuondoa kipengele cha Trending Topics hivi karibuni

1-EntryPoint-2UP-EN

Kwa mujibu wa mtandao wa Mashable, watu mashuhuri kama Selena Gomez, Kim Kardashian na Kevin Hart tayari wamekwisha jisajili kama partners wa Instagram IGTV na tayari wameanza kupakia video zao.

Pia hatukuwa nyuma kwani tayari tuna channel yetu ya instagram.com/mtaawasaba ambapo tutaweka video mpya muda si mrefu. usisahau kutembelea ili kuona video za mambo mbalimbali ya teknolojia kwa urefu.

Usikose Kusoma:  Vita ya simu zinazokunjika: Hii ndiyo Huawei Mate X

2-Watch-2UP-EN

Tunasubiri tuone ni jinsi gani Instagram wamejipanga kupambana na YouTube ambayo kwa sasa ndio mfumo mkubwa kabisa duniani wa upakiaji wa video.

Pia kupitia blog yao, Instgram wametangaza kufikisha watumiaji hai takribani bilioni moja mpaka sasa. Hii inafanya mtandao huu wa kijamii kuwa ndio unaoongoza kuwa na watengenezaji vipindi wengi kuliko zingine zote duniani, jambo hili linawezesha kuwepo kwa fursa kwa watumiaji kujiingizia kipato kupitia video ambazo watakuwa wakitengeneza, jambo linategemewa siku zijazo hasa kupitia IGTV.

Instagram-1-billion-users

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa