Motorola RAZR kurudi mwaka huu ikiwa na kioo kinachojikunja

Ripoti kutoka tovuti ya Wall Street Journal inasema, kampuni ya Motorola ambayo kwa sasa iko chini ya Lenovo ya China, iko mbioni kuachia toleo jipya la simu ya Motorola RAZR. Simu hii mpya inatarajiwa kutoka mwezi wa pili mwaka 2019 na itakuja na kioo kinachojikunja kama simu ya Samsung Galaxy F. Toleo hili linatarajiwa kuingia sokoni kwa bei ya kuanzia dola za kimarekani 1500.

Usikose Kusoma:  Android Go Edition: Android Oreo kwa simu za hali ya Chini

Simu ya RAZR ilijipatia umaarufu mkubwa miaka hiyo kwa muonekano na uimara wake. Kwa sasa Motorola wanashirikiana na kampuni ya simu ya Verizon kufufua brand ya RAZR, ambapo mwaka 2011 na 2012 walijaribu kurudisha simu ya Droid RAZR.

Katika maombi ya hakimiliki ya teknolojia ya simu iyo mnamo mwaka jana, michoro inaonesha simu hiyo itakuwa na kioo kinachojikunja kuelekea ndani ikifananishwa na simu kadhaa zilizotoka au ambazo ziko mbioni kutoka hasahasa Samsung Galaxy F.

Usikose Kusoma:  Samsung Experience 9.0 yaja na maboresho ya Emoji

Hata hivyo sio kampuni ya Motorola pekee inayorejesha msisimko wa simu zao zilizovuma miaka hiyo. Tumeona Nokia wakiwa chini ya HMD Global wakiachia simu kama 3310 na 8110 maarufu kama banana phone

 

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa