Ni namna gani e-SIM itabadilisha mfumo wa teknolojia kuwa bora zaidi

Apple, Samsung na Google imeanza mazungumzo kwa watoa huduma zamitandao kuhusu kupitisha kadi za umeme (electronic SIM) kwa ajili ya smartphone za baadae. Samsung ndiyo kampuni ya kwanza ilianza kutumia huduma ya GSMA kuwezesha e-SIM kwenye kifaa cha Samsung Galaxy Gear S2, na mwanzoni mwa mwezi wa tisa mwaka huu Apple nao imeangazia huduma hiyo na kuiwezesha katika baadhi ya vifaa vyake zikiwemo Apple Watch series 3 na iPad, Google mwanzoni mwa mwezi wa kumi nayo ikatoa kifaa chake Google Pixel 2 zenye kuwezeshews kutumia huduma hiyo ya e-SIM.

Lakini ni Nini hasa Maana ya e-SIM?

Neno e-SIM (Electronic Subscriber Identity Module) linahusiana na kiwango kipya cha Teknolojia ya GSMA – Chama kinachowakilisha waendeshaji wa huduma zamitandao duniani kote, Kadi ya kielectroniki.

e-SIM inakuja kwa mfumo wa CHIP jumuishi ambayo haiwezi kabisa kuondolewa (Not Removable) katika Mfumo mzima wa simu, Naweza kusema inakuwa manufactured na aina ya yasimu husika, unakuwa huna tena uwezo wa kubadiri SIM-Card kwenye simu yako.

Mpaka sasa umeshaanza kupata japo mwanga nini maana ya e-SIM,? Kama jibu ndiyo tuendelee sasa,

Kwa vivyo mtumiaji atakaenunua kifaa hicho ataweza kuunganishiwa huduma zake za kimawasiliano moja kwa moja kwenye simu yake bila kuto kuwa na haja ya kiubadiri SIM-Card.

Usikose Kusoma:  Motorola RAZR kurudi mwaka huu ikiwa na kioo kinachojikunja

Kampuni ya Zantel hapa Tanzania ndiyo iliweza kutumia huduma hiyo hasa katika vifaa vyake vya mtandao wa data USB – Modem kupitia mtoa huduma wake mkuu wa mtandao Etisalat.

Faida/Hasara za e-SIM katika jamii yetu.

Tumeitazamia huduma hii kama tulivyoielezea hapo juu sasa tukiangalizia katika faida na hasara za huduma hii ya e-SIM,

Tumekuwa na matukio mengi sana kuhusu wizi wa simu za mikononi, kwa upande mwingine tunawza sema hii ni moja ya faida kwa haitamuwezesha aliyeiba kwenda kubadiri sim card na kuweka yakwake au kutoa sim card yako ukose mawasiliano, kwa maana hiyo basi itamlazimu kuizima simu hiyo, na pindi atakapohitaji kuitumia simu hiyo itamlazimu ku-swap mawasiliano na itamhitaji kwenda kwa mtoka huduma za mitandao na hapo itakuwa rahisi ,mtu huyo kuwekwa mikononi mwa sheria.

Changamoto huja kwa wale watumiaji wa namba za simu tofauti tofauti kwa huduma hii itakufanya kutumia mtoa hudua mmoja tu wa matandao kwa kipindi kirefu hadi pale utakapohitaji kwenda kubadirisha kwenda kwa mtoa huduma mwingine wa mtandao Kama kuhama Tigo kwenda Vodacom hii pia itakuwa ni changamoto kubwa kwa watumiaji.

Je umeipenda hii? tafadhari andika maoni yako hapo chini kwa kujaza email yako najina kamili!

Tufuatilie @MtaawaSaba ili usipitwe na matukio mbali mbali ya mitanadoni na ya kiteknolojia kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Google+ na Youtube, Pia usisite kutoa maoni yako kwa mhariri@mtaawasaba.com

Maoni 1

  1. Teknolojia hii ya e-SIM itakuwa changamoto kubwa sana huku Africa.pia ukiangalia mitandao yetu huwa sometime inasumbua network inapelekea ukitaka ubadili lain kwa muda huo upate huduma inakuwa mtihani.

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa