Nokia 9 PureView yenye kamera tano yazinduliwa kwenye maonesho ya MWC 2019

HMD Global wamezindua simu janja ya hadhi ya juu ya Nokia 9 PureView. Simu imegusa vichwa vya habari kwa kuwa ndio simu janja ya kwanza duniani kuwa na kamera tano upande wa nyuma zote zikiwa na sensa za megapikseli 12.

Kampuni hiyo inayotengeneza simu zenye jina la Nokia imejinadi ikisema  “kila picha inayopigwa na Nokia 9 PureView iko kwenye mfumo wa HDR, na kamera zote tano zinapiga picha kwa pamoja na kisha kuziunganisha ili kupata picha moja yenye megapikseli 12 iliyo na ubora wa kipekee”

Usikose Kusoma:  Apple waachia iOS 11.2.6 kutatua tatizo linaloharibu iPhone

Simu hii inalenga wapiga picha na washabiki wa upigaji wa picha zenye ubora mkubwa. Simu inakubali kutoa picha katika mfumo wa RAW, pia inafanya kazi na app kama Adobe Lightroom mahususi kwa ajili ya kuhariri picha zako moja kwa moja kutoka kwenye simu yako.

Nokia-9

Sifa za Kamera

Kamera tatu zinapiga picha zenye rangi moja, huku zilizobaki mbili zinatoa picha za rangi kabla picha zote hazijaunganshwa pamoja.

Kamera hizi zina uwezo wakuondoa chenga chenga kwenye picha hata kama utazoom hii inaleta ubora zaidi kwenye picha.

Usikose Kusoma:  Kufa kwa symbian neema kwa asha sasa yapata multitasking na swipe ui

Software kwa upande wa kamera pia imeboreshwa zaidi ili kuhakikisha uchakataji wa picha unakuwa maridhawa.

Sifa za simu ya Nokia 9 PureView

Nokia 9 PureView
vipimo155 x 75 x 8 mm (172g)
mfumo endeshiAndroid 9.0
kioo5.99-inch QHD+ OLED
ProsesaQualcomm Snapdragon 845
RAM6GB
hifadhi128GB
Kamera yuma5 x 12MP f/1.82 (2 x RBG, 3 x Mono)
Kamera ya mbele20MP
MuunganishoWi-Fi 802.11ac, Bluetooth 5.0
MawasilianoLTE Cat. 16 4×4 MIMO
aina ya chajaUSB-C
uwezo wa kutoingia majiIP67
ulinzi In-screen fingerprint scanner
Betri3,320mAh

 

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa