Sasa kupitia WhatsApp unaweza kupiga simu za sauti na video kwa hadi watu wanne

Kampuni ya WhatsApp leo imefanya maboresho kwenye huduma yake ya kutuma na kupokea jumbe, ambapo sasa watumiaji wataweza kufanya video calls kwa vikundi, yaani watumiaji hadi wanne sasa wataweza kuongea kwa pamoja, hii ni kwa watumiaji wa iOS na Android.

Ili uweze kutumia huduma hii mpya ni lazima uanze kwa kuongea na mtu mmoja kwanza, kisha kitaibuka kitufe cha kuongeza washiriki wa mazungumzo hayo upande wa juu kulia mwa skrini yako kama inavoonekana kwenye video fupi hapo chini.

Usikose Kusoma:  Apple imetangaza kuboresha Programu za iPhoneX

Ikumbukwe maboresho haya yyalianza kutajwa mwezi wa tano kwenye kongamano la Facebook F8 developer conference, WhatsApp walitangaza kuwa wataachia huduma ya kupiga simu za kawaida na za video kwa vikundi miezi michache ijayo. Leo wamethibitisha hayo na huduma iyo tayari imeanza kupatikana duniani kote kwa watumiaji wa Android na iOS.

Huduma hii iko encrypted kama ilivyo kwenye jumbe za maandishi, hii inafanya isiwezekane kwa mtu mwingine kudukua mazungumzo wa sauti au video kwa watumiaji wa WhatsApp.

Hakikisha una update app yako ya WhatsApp ili uweze kuona maboresho haya mapya yatakayokuwezesha kupata huduma izo mpya.

Usikose Kusoma:  Instagram yazindua IGTV, programu tumishi kwa ajili ya video ndefu.

Ahsante kwa kufuatilia habari hii, Pia usisiste kutoa maoni yako hapo chini, na usisahau kuSubscribe katika Chanel yetu ya Youtube  uweze kupata video za kila wiki kupitia youtube. Kwenye mitandao ya kijamii instagram, twitter na facebook tufuate @Mtaawasaba

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa