Serikali kumiliki hisa zaidi za Airtel Tanzania

Kwa mujibu wa tovuti ya gazeti la kila siku la Mwananchi, makubaliano ya Serikali ya Tanzania kuongeza hisa zaidi za umiliki wa kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tanzania yamefikiwa leo Ijumaa Januari 11, 2019 baada ya mazungumzo kati ya Rais John Magufuli na mwenyekiti wa kampuni ya Bharti Airtel Sunil Mittal, waliokutana Ikulu Dar es Salaam.

Kampuni ya Bharti Airtel ya India ambayo ndio mmliki mkuu wa kampuni iyo, imekubali kuongeza hisa zinazomilikiwa na Serikali ya Tanzania  kutoka asilimia 40 hadi 49. Kwa uamuzi huo wa kuongeza hisa zinazomilikiwa na Serikali ya Tanzania, utafanya hisa zinazomilikiwa na Bharti Airtel kutoka asilimia 60 hadi asilimia 51.

Usikose Kusoma:  Google yanunua sehemu ya HTC kwa dola bilioni 1.1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisoma taarifa ya majadiliano kutoka kwa mgeni wake Bw. Sunil Mittal Mwenyekiti wa Bharti Airtel ( kampuni ya Simu ya Airtel ) mara baada ya Mazungumzo yao . Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 11,2019.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Magufuli na Bwana Mittal wamefurahishwa na hatua waliyofikia katika mazungumzo hayo pamoja na kuongeza hisa za Serikali katika umiliki wa Airtel Tanzania, ambapo Mittal amesema kampuni yake imeridhishwa na makubaliano yaliyofikiwa katika masuala yaliyokuwa yakijadiliwa yenye lengo la kuiimarisha kampuni ya Airtel, kuleta manufaa kwa pande zote mbili na kuboresha huduma za mawasiliano za kampuni hiyo.

Usikose Kusoma:  Bakhresa kuja na Azam Telecom

Rais Magufuli alinukuliwa akisema “Masuala mengine ya kumalizia mazungumzo haya yataendelea leo ili kumalizia, lakini jambo zuri ni kuwa sasa wamekubali kutoa gawio kwa Serikali ambapo kwa muda wa miaka minane hadi kumi tulikuwa hatujapata gawio,” hii ni baada ya kampuni hiyo kukubali kutoa gawio kwa Serikali ya Tanzania pindi mazungumzo hayo yatakapomilika hivi karibuni.

Timu ya majadiliano kati ya serikali ya Tanzania na kampuni ya Bharti Airtel inaongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa  Palamagamba Kabudi.

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa