Simu 5 zinazokunjika zinazotegemewa kutoka 2019

Mwaka wa 2018 ulikuwa ni mwaka wa fasheni ya notch kwa simu zilizotoka mwaka huo. Mwaka huu wa 2019 tunaona ni mwaka wa teknolojia wa simu na vifaa vyenye vioo vinavyokunjika ama kizungu foldable screens.

Mpaka sasa makampuni kadhaa yametangaza na baadhi yako kwenye hatua tofauti tofauti katika kutimiza azma ya kuachia simu simu zinazokunjika. Mpaka sasa hakuna hata moja ambayo iko tayari kwa soko la watumiaji wa kawaida.

Hebu tuangalie simu tano ambazo tuna uhakika zitaachiwa mwaka 2019

Royole Flexpai

flexpai-1-5-1220x813

 

hii ndio simu janja ya kwanza kabisa duniani inayojikunja. ilitangazwa oktoba 31, 2018 huko Beijing China, simu hii imeleta picha ya namna simu za namna hii zitakavokuwa.
Simu hii inakuja na  prosesa ya Snapdragon 855 ambayo ina uwezo mkubwa sana wa kufanya kazi mbalimbali pale unapokuwa simu na pale inapokuwa tablet.
Inakuja na RAM ya GB6 pamoja na hifadhi ya ndani GB128, pia inakuja na machaguo mengine ya RAM ya GB8 na hifadhi ya GB256 na toleo linakuja na RAM ya GB8 na hifadhi ya GB512.

 

Simu ina betri yenye uwezo wa 3970mAh, ina port ya USB-C na fingerprint scanner. Haina sehemu ya kuchomeka headphone na ikamera mbili nyuma zenye 16mp na 20mp. Kioo chake ni AMOLED chenye resolution ya 1920 x 1440.
Simu hii ya Royole FlexPai itaanza kuuzwa nchini China kwa Yuan ya China 9,000 ambayo ni sawa na shilingi za kitanzania takribani 2,972,000 bila kodi.

Samsung Galaxy Fold

fold-butterfly

(updates) Simu-Tableti yenye kioo cha kujikunja ya Samsung Galaxy Fold hatimaye imezinduliwa kwenyetukio la Galaxy unpack pamoja na simu za familia ya Galaxy S10, hii ni baada ya miaka ya kusubiri na tetesi kibao kuhusu simu hii. Ili uweze kuimiliki simu hii ni lazima toboke mfuko maana bei yake ni dola za kimarekani takribani 1980 sawa na shilingi za kitanzania 4,642,000 hivi.

Usikose Kusoma:  Samsung yazindua Diski ya SSD yenye ukubwa wa Terabyte 30

Hizi ni baadhi ya sifa za simu hii:

  • Ukubwa wa kioo: 4.6-inch Super AMOLED; 7.3-inch QXGA+ Dynamic AMOLED
  • Mfumo endeshi: Android 9.0 with Samsung One UI
  • Kamera: 16-megapixel (ultra-wide-angle), 12-megapixel (wide-angle), 12-megapixel (telephoto)
  • Kamera upande wa mbele: Two 10-megapixel, 8-megapixel 3D depth
  • Prosesa: Octa-core Qualcomm Snapdragon 855
  • Hifadhi: 512GB
  • RAM: 12GB
  • Memori kadi: None
  • Betri: 4,380 mAh
  • Fingerprint sensa: upande wa kulia

 

Motorola RAZR 2019

moto-razr-2019-patent-1-900x600-c

Kwa mujibu wa ripoti kutoka tovuti ya Wall Street Journal inasema, kampuni ya Motorola ambayo kwa sasa iko chini ya Lenovo ya China, iko mbioni kuachia toleo jipya la simu ya Motorola RAZR. Simu hii mpya inatarajiwa kutoka mwezi wa pili mwaka 2019 na itakuja na kioo kinachojikunja kama simu ya Samsung Galaxy Fold. Toleo hili linatarajiwa kuingia sokoni kwa bei ya kuanzia dola za kimarekani 1500.

Usikose Kusoma:  Android Go Edition: Android Oreo kwa simu za hali ya Chini

Motorola inachofanya kurudisha msisimko wa Simu ya RAZR iliyojipatia umaarufu mkubwa miaka hiyo kwa muonekano na uimara wake kama ambavyo simu za Nokia 3110 zilivorushwa na HMD Global kukunbushia matoleo ya awali yaliyofanya vizuri.

 

Huawei Mate X

huawei-mate-x-leak

Huawei pia hawako nyuma katika teknolojia hii ya simu zinazojikunja. Mapema walitangaza kushugulika na simu zinazojikunja na hakukuwa na taarifa zaidi ya simu itakuwa ya kujikunja na itakuwa na uwezo wa 5G. Katika picha iliyovuja imeonesha jina la simu kuwa ni Huawei Mate X huku ikionesha simu ikiwa imefunguliwa, imefunguliwa nusu, na imefungwa. Simu hii inatarajiwa kuzinduliwa kwenye maonesho ya MWC 2019 ikiwa ni siku chache baada Samsung kuzindua simu yao inayojikunja.

 

Xiaomi

xiaomi-foldable-device-twitter

Msemaji wa Xiaomi, Donovan Sung alichapisha video kwenye Twitter, akionyesha mwanzilishi wa Xiaomi, Bin Lin akicheza na simu inayoonekana inajikunja. Mtendaji pia aliuliza watumiaji kuja na jina la kifaa hiki kipya.

Hakuna taarifa nyingi kuhusu simu hii ambayo kwa sasa ni prototype. zaidi kuwa ina uwezo wa kujikunja mara tatu.

Endelea kuwa nasi kwa kutufuata kwenye mitandao ya kijamii na kwa njia ya barua pepe ili usikose habari pindi zinapotoka.

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa