Simu mpya za Huawei zazuiwa kupakua app ya VLC

Simu mpya za Huawei haziwezi tena kupakua tena app maarufu ya  VLC for Android kutoka kwenye duka la app la Play Store, yote haya yamesababishwa na ROM inayotumika kwenye simu za Huawei maarufu kama EMUI inayozuia app kufanya kazi kichini chini.
Watengenezaji wa App hii maarufu mahususi kwa ajili ya kuangalizia video na ku stream, wamefikia maamuzi haya ya kuzuia simu hizi mpya Huawei baada ya kupata malalamiko makubwa kwa watumiaji wa simu hizo, na wengi wao wakiacha negative review kwenye Google Play Store kuhusu app hiyo.

Simu za Huawei zinazokuja na toleo jipya la ROM hiyo ya EMUI huua app ambazo zina endelea kufanya kazi hata baada kuiondoa kwenye screen. Hatua hiyo ni kwa ajili ya kuokoa matumizi ya RAM kwenye simu na kuokoa chaji kwenye simu.

Usikose Kusoma:  Tigo, Selcom na Mastercard waungana kuleta huduma ya Masterpass QR nchini Tanzania

Katika tweet iliyoandikwa kwenye akaunti ya VideoLAN, ambao ndio watengenezaji wa app ya VLC wamesema wamefikia maamuzi hayo kutokana na sera ya Huawei kufunga app zinazorun kwenye background kitu ambacho kinasababisha app ya VLC kutotoa sauti pindi inapotumika kichinichini.

Tweet hiyo pia ina viunga vinavyoelekeza kwenye tovuti ya mijadala ya VLC ikionesha baadhi ya watumiaji waliokasirishwa na kitendo cha kuua app zinazorun kichinichini huku ikiacha zile za Huawei bila kuzifunga. Na kuwasababisha kufikia maamuzi hayo.

Usikose Kusoma:  Hakuna tena majina ya vyakula, toleo jipya la Android litaitwa Android 10

Hata hivyo watumiaji wa simu za awali za Huawei wataendelea kuipata VLC bila wasiwasi japo sio kwa simu zote. Pia inawezekana kupakua app ya VLC moja kwa moja kutoka kwenye tovuti yao.

watumiaji wa simu mpya Huawei watakumbana na ujumbe huo pindi watakojaribu ku download app ya VLC

Mpaka sasa simu ambazo zimethibishwa kukumbwa na kadhia hii ni  pamoja na Huawei P8, P10, bila kusahau Huawei P20, japo watumiaji wake wanaruhusiwa kudownload kutoka kwenye tovuti ya VLC.

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa