Twitter sasa yatambua Kiswahili kama lugha rasmi

Mtandao wa kijamii wa Twitter umeongeza lugha ya Kiswahili kama moja ya lugha rasmi kwenye mtandao huo. Kiswahili ni moja ya lugha zinazotumika na watu wengi zaidi Afrika ikizungumzwa na watu zaidi ya milioni 200, hatua hii imekuja baada ya kampeni ya taasisi ya eNitiate, inayojihusisha na mambo ya mtandao, kudai kupewa nafasi sawa kwa lugha za kiafrika kwenye mtandao huo wa kijamii.

Usikose Kusoma:  Viongozi wa makundi ya Whatsapp watakiwa kutoa taarifa za uhalifu

Hapo awali mtandao huo wa kijamii ulikuwa ukitafsiri maneno ya kiswahili kama ya kiindonesia. Sasa inaungana na mitandao mingine mikubwa ya kijamii ya Marekani kama Google, Facebook na Wikipedia kutambua lugha ya Kiswahili kma alugha rasmi.

Taasisi iyo ili tweet siku y alhamisi yaliyojiri baada ya kampeni yao kuanza;

“Tumepiga kelele, kelele nyingi; kuhusiana na #SwahiliIsNotIndonesian na #TwitterRecognizeSwahili. Tunashukuru kwa Twitter kutusikiliza. Tunashukuru kwa kutambua Swahili,” waliandika Brand Kenya

Usikose Kusoma:  TECNO kuja Na Camon CM January hii

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa