YouTube Music: Huduma mpya ya kustream muziki kutoka Google yazinduliwa

Leo YouTube wanazindua huduma mpya kustream muziki iliyopewa jina la YouTube Music. Huduma hii itakupa fursa ya kusikiliza albamu nzima, cover, remix, matoleo ya live pamoja na stesheni za radio za wasanii kwenye app za simu na kompyuta. Kwa kutumia teknolojia ya kisasa utaweza kuchaguliwa au kushauriwa nyimbo za kusikiliza kutokana na aina ya muziki unayopenda kusikiliza.

Huduma hii mpya ya kustream muziki ya YouTube inakuja kupambana na huduma zingine ambazo zipo tayari zinazotoa huduma ya ku stream muziki ikiwemo Spotify, Apple Music, na Amazon Music. YouTube Music itafuata mfumo wa wapinzani wao wanaotoa huduma za kustream muziki ambapo kuna watumiaji watapata huduma bure na matangazo ya biashara, pia kwa kulipia ambapo utapata huduma bila matangazo.

Usikose Kusoma:  Samsung Galaxy Fold: Kwanini usubiri toleo linalofuata

YouTube-Music

Watumiaji waliojisajili kwa ajili ya Google Play Music watakuwa moja ya watu wa kwanza kabisa kupata huduma hii mpya, kuna ripoti zinazosema kwa sasa Google Play Music inaondolewa na huduma zake zitapatikana kwenye YouTube Music.

Pia imejulikana kwamba YouTube Red, huduma ya kulipia ya kuona video za YouTube bila matangazo na vitu vingine zaidi ambavyo wanaoona version ya kawaida hawapati, inabadilishwa jina na kuwa YouTube Premium. Huduma hii mpya itaruhusu mtumiaji kupata huduma za YouTube Music. Kwa watumiaji wapya watajisajili kwa gharama ya dola za kimarekani 11.99 ambayo ni zaidi ya gharama ya sasa ya kujisajili.

Usikose Kusoma:  Huu ndio muonekano wa Samsung Galaxy S10

Nchi ambazo zitakuwa za kwanza kuifaidi huduma hii mpya ni pamoja na Marekani, Mexico, Australia, New Zealand, bila kusahau Korea Kusini. Pia YouTube imesema Nchi zingine ambazo zitaongezewa kwenye orodha kuanzia juma lijalo ni pamoja na Austria, Canada, Denmark, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Ireland, Italy, Norway, Urusi, Hispania, Sweden, Uswizi, na Uingereza.

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa