Zuckerberg achapisha ukurasa mzima kwenye gazeti kuomba radhi juu ya kashfa ya Cambridge Analytica

ZuckìKufuatia kashfa kubwa ya uvunaji wa taarifa za watumiaji wa mtandao wa kijamii uliofanywa na kampuni ya Cambridge Analytica iliyosababisha kushuka kwa kasi ya ajabu hisa za Facebook kwenye soko la hisa Marekani. Mkurugenzi mtendaji wa Facebook na viongozi wengine wa juu wa kampuni hiyo wameendelea kuomba radhi kwa watumiaji wa mtandao huo wa kijamii. Wamekuwa wakifanya mahojiano na runinga mbalimbali, na machapisho mengine kuelezea ni jinsi gani walivosikitishwa na tukio hilo. Kujulikana kwa kashfa hiyo kumechochea kaulimbiu ya #DeleteFacebook inayohamasisha watu waondoe taarifa zao na kufunga kabisa akaunti zao za Facebook.

Usikose Kusoma:  Kila kitu unachotakiwa kujua kuhusu Samsung Galaxy S10, S10 Plus, S10e, na S10 5G

Facebook-Cambridge-Analytica-Apology-AP-Image

Katika hali ya kushangaza, Facebook wameamua kuweka tangazo kwenye magazeti ya The Observer, The Sunday Times, Mail linalotoka jumapili, Sunday Mirror, Sunday Express na Sunday Telegraph kwa upande wa uingereza, wakati kwa upande wa Marekani walichapisha tangazo hilo kwenye magazeti ya, The New York Times, The Washington Post, na The Wall Street Journal ikiwa ni baadhi ya magazeti waliyoweka tangazo la kuomba radhi wananchi. Tangazo hilo limesainiwa na mkurugenzi mtendaji Zuckerberg, kwa mkono wake. Likisisitiza watajitahidi kuboresha namna wanavotumia taarifa za watumiaji wao.

Kama sehemu ya radhi yanayoomba, wamesema tayari facebook imebadili sera ya uvunaji taarifa za watumiaji kufuatia sintofahamu iliyotokana na app ya “every single app” na wanafanya uchunguzi wa kina kuelewa ni namna gani app hiyo ilifanikiwa kuvuna taarifa nyingi kiasi hicho. Katika tangazo hilo wanasisitiza, watapiga marufuku app zote za namna hiyo katika mtandao wao na zote ambazo zitaonekana kukiuka sera zilizowekwa.

Usikose Kusoma:  Samsung Galaxy S9: kuzinduliwa Februari 25

Kufuatia kashfa hiyo hiyo ya uvunaji taarifa za watumiaji na Cambridge Analytica. Mkurugenzi mtendaji Zuckerberg anatakiwa akatoe ushahidi  kwenye kamati House Energy and Commerce Committee mbele ya baraza la Congress.

Wakati huohuo kampuni iliyosababisha kashfa hii ya Cambridge Analytica imeanza kufanyiwa uchunguzi ambapo makao makuu yao huko uingereza yalivamiwa ijumaa iliyopita.

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa