Gari lisilokuwa na dereva la Uber lagonga na kuuwa.

Kampuni ya Uber imesitisha majaribio ya magari yake yasiyokuwa na dereva huko amerika ya kaskazini baada moja ya magari yake lililokuwa linajaribiwa huko Jimbo la Arizona, Marekani kumgonga mpitanjia na kumsababishia kifo.

Tukio hili limewalazimu  Uber kusitisha kwa muda majaribio yao mengine ya magari yasiyokuwa na dereva waliyopanga kuyafanya kwenye miji Phoenix, San Fransisco, Pittsburgh na Toronto. Inaaminika hii ndo ajali mbaya kuwahi kutokea ikihusisha teknolojia ya magari yasiyokuwa na dereva.

Msemaji wa mamlaka ya bodi ya usafiri huko nchini marekani bwana Erick Weiss amesema wameanza kufanya uchunguzi pia Mkurugenzi Mkuu wa Uber pia amesema kampuni yake nayo inachunguza kuona ni nini hasa kilitokea.

Gari hili lililokuwa linajiendesha lenyewe lilisababisha ajali mbaya ingawa palikuwa na dereva ndani wa hilo kuliongoza kama mambo yakienda mrama, ripoti ya polisi wa mji wa Tempe, Arizona ilieleza hivyo. Ajali ilitokea saa nne usiku karibu na njia panda iliyo na njia nyingi. Polisi wanaendelea kusema gari la Uber lilikuwa linakuja barabara ya curry ambapo mwanamke alitambulika kama Elaine Herzberg alikuwa anavuka akitokea upande wa magharibi mwa barabara ndipo alipogongwa na alifariki hospitali.

Magari haya yasiyokuwa na dereva yamekuwa yakitengenezwa na kampuni kubwa za teknolojia huko marekani, mfano waymo zamani ilijulikana kama project ya google kwa magari ya aina hii na yalikuwa yanaonekana sana Jimbo la Arizona. Kampuni kubwa za kutengeneza magari kama Ford, Volvo, Tesla, Toyota, General Motors pamoja kwa nyakati tofauti yamekuwa yakibuni, tumia, na kujaribu teknolojia hii. Kati ya hao, kampuni 50 zimeomba na kupatiwa kibali kwenye Mamlaka za mji wa California kujaribisha magari ya aina hii mradi tu pawe na dereva wa akiba ndani wa kuliangalia lisifanye uharibifu na hata kusababisha vifo tena wa watuamiaji wengine wa barabara. Mwezi kesho sheria mpya itawekwa katika Jimbo la California kuruhusu kampuni hizi za teknolojia kujaribu na kutumia magari haya bila kuwa na dereva ndani iwapo watafikia vigezo ambayo Idara na Mamlaka za usafirishaji imeweka.

WAWEZA SOMA:  Samsung Galaxy S9: kuzinduliwa Februari 25

Wadau na Maafisa wa usafirishaji nchini marekani wameomba sheria kali itungwe juu ya magari ya aina hii, sheria ambayo itawalinda na kuomba wahusika kuchuliwa hatua kali zakisheria kama magari yao yateendelea kujaribiwa na kuendelea kuuwa wapendwa wao. Wengine walipendekeza majaribio hayo yakifanyika wananchi wataarifiwe ili wawe makini watumiapo hizo barabara hili naona litasaidia kuokoa maisha ya watu. Wakosoaji wengine wameenda mbali na kusema hizi kampuni ni kama zinawahi kujaribu teknolojia zao huku bado hawajaridhisha kama kweli ni rafiki kwa binadamu, ila wataalamu wa teknolojia wamesema kwenye majaribio hasa ya aina hii lolote linaweza tokea linaweza kufaulu vyema au kufeli pia. Miss Cummings, mtaalamu wa robotics katika chuo kikuu cha Duke ambaye amekuwa muhimu sana katika teknolojia hii amesema mifumo ya maono ya kompyuta ya inayotumika kuendeshea haya magari ni mbaya sana, mara nyingi sio ya kuiamini nadhani watafiti inatubidi tutafute mbinu ya kuboresha hii kwanza.

Mwishoni mwa mwaka 2016 Gavana wa Arizona bwana Doug Docey alisaini sheria ya kuruhusu kampuni za teknolojia kuja kufanya kazi zao jimboni kwake baada ya kuona zinabanwa sana na Mamlaka za California. Tangu sheria hiyo ianze kufanya kazi Jimbo hilo limekuwa likipokea kampuni nyingi sana zinazotaka kufanya kazi, au kujaribu bidhaa zao mfano Uber na haya magari yao yasiyo na dereva yamekuwa yakijaribishwa sana.

Ingawa Arizona imefungua mlango wake kwa hizi kampuni, basi inajukumu kubwa la kuhakikisha wakazi wa mji huo wako salama kipindimajaribio ya aina hii yanapotokea. amesema Cumming. Kampuni hizi zimeeleza kwamba kabla ya kujaribisha haya magari eneo litakalo tumika wanali-scan, kabla ya kuruhusu magari yao na ramani ya hapo inatumwa kwenye mfumo wa gari husika. Kamera zilizofungwa zinakisaidia chombo kuwa makini na vitu vinavyoizunguka pia ramani na drones zilizopo juu ya chombo pamoja zinasaidiana kutambua vitu mbalimbali, ikiwemo majengo, sehemu za mapumziko, alama za pundamilia, taa za barabarani, watumiaji wengine wa barabara nguzo, miti, iliyopo mwanzoni na katikati ya barabara.

WAWEZA SOMA:  Ubora wa Apple iPhone 8, 8 Plus na iPhoneX

Lakini, kupata ramani ya eneo husika na chombo kuweza kutambua baadhi ya vitu haina maana kwamba uko salama inatakiwa tuchukue tahadhari sababu kama kweli hii teknolojia ni nzuri  basi Elaine Herzberg asingegongwa maana yeye alikuwa anavuka barabara aliporuhusiwa na kuongozwa na taa, aliongeza Cumming.

Ubora wa kamera ndani ya magari haya, sio mzuri wa kuweza kutambua umbo, na watumiaji wengine barabara katika mda na wakati huo huo hii moja kati ya changamoto ambayo Wahandisi wa teknolojia hii wanapaswa kuangalia kwa jicho la tofauti na kuleta ufumbuzi.

Timothy Carone Profesa msaidizi anayefundisha mifumo ya teknolojia hizi katika chuo cha Notre Dame  amesema ajali hizi zinazohusisha vyombo hivi visivyo na dereva ni mbaya sana ila muhimu majaribio yakaendelea kwenda mbele na kwa ukubwa zaidi.

Majaribio ya barabarani ndo njia pekee mifumo ya magari haya itawasaidia wahandisi kujua wapi kuna shida na nini kifanyike vyombo hivi viweze kuendana na mazingira tunayoishi. Pia yatasaidia sana kupunguza vifo kama tutafanikiwa kwa asilimia 100% huko mbele.

Ndio, nafahamu kwa sasa itakuwa ni ngumu sana kukubali vifo hivi vinavyotokea kipindi hiki cha majaribio ya teknolojia hii ila mda si mrefu tutaanza kuona mwanga. Nawahakikishia kwamba teknolojia hii ikifanikiwa itafanikiwa kuokoa vifo vingi sana vya barabarani na tunahitaji kufika huko, alisema Profesa Carone.

 

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa