Google washirikiana na Levi’s kutengeneza koti la kidigitali.

Google kama tuijuavyo imekuwa ikibuni bidhaa mbalimbali kwa miaka mingi sana vitu kama simu, tarakilishi mpakato (laptop), spika, VR goggles, vifaa vya masikioni (ear buds) na kamera, je wadhani ni kipi bado? Nadhani utajiuliza ni nini?

Google kwa kushirikiana na levis wameweza kutengenea koti la kidigitali. koti hili limetengenezwa mahususi kwa waendesha baiskeli, pikipiki na hata madereva ambao wawapo barabarani mikono yao ipo bize kwenye usukani na sio kwenye simu zao.

Hili koti, linaonekana la kawaida kama yale matoleo mengine ya levis yaliyopita ila hili linatofauti chache mpya.

Koti hili lina mifuko miwili mbele kifuani na mmoja uko chini ya bega kushoto wenye zip itoshayo kabisa kuhifadhi vitu vyako, pia ina reflector itakayokusaidia kuonekana hata  usiku  na watumiaji wa barabara bila kusahau material ya hili koti inavutika kwa maana ya kwamba mvaaji akijikunja wakati anaendesha pikipiki au baiskeli lisimbane na kumkosesha raha hasa hasa mgongoni na tumboni.

Tofauti kubwa ya hili koti, ambayo imefichwa na sio rahisi kuonekana chini kwenye mkono wa kushoto levis pamoja na google wameweka kitambaa ambacho ni touch-sensitive kilichopo juu ya kiganja (left cuff) kwenye hili koti kilichobuniwa mahususi kwa ajili ya kazi hii. Kifaa hiki kinapokea ishara na kikiguswa pia hutoa chaguo mbalimbali.

Google wameweka soketi ya umeme kwenye ambayo inaiwezesha koti kufanya kazi zake vyema pia wamebuni kifaa kidogo wamekiita snaptag chenye material ya mpira, chembamba sana urefu wake ni inchi tano. Kifaa hiki (snaptag) kina betri, bluetooth, vibration mdule na LED light. Unapotaka kukichaji unakichomoa pale kwenye soketi ya umeme iliyopo kwenye koti lako, halafu unakichaji kwenye USB port iliyopo kwenye tarakilishi (computer) yako kikijaa unachomoa na kukirudisha kwenye koti lako na kwa kawaida inachukua wiki mbili cha chaji kuisha na kuchaji upya. Hiki kifaa (snaptag) ni kama central processing unit ya hili koti bila hiki kifaa koti lako halina maana.

WAWEZA SOMA:  Instagram yazindua IGTV, programu tumishi kwa ajili ya video ndefu.

Download application ya Jacquard kwa watumiaji wa Android au IOS halafu unganisha snaptag na simu yako. Kifaa hiki kinakupa uwezo wa kutumia hadi ishara nne bila kusahau pia kwa kutumia application ya Jacquard unaweza kusikiliza muziki, ina GPS inayoweza kukuonyesha mahali upo na kukuelekeza pahali, inakusomea muda, inakusomea meseji, ukisahau simu yako kifaa hiki kitakusaidia kuitafuta kwa kutuma signals na simu itawaka na kuiona, pia inawaka na ku-vibrate kama utapigiwa au kutumia ujumbe mfupi wa maneno.

Subscribe Chanel yetu ya YouTube uweze kupata habari zaidi za teknolojia.

 

 

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa