Google yanunua sehemu ya HTC kwa dola bilioni 1.1

Mwandishi Alexander Nkwabi

Hatimae yamekuwa, yale yaliyokuwa yakizungumzwa kwa miezi kadhaa kuhusu google kuinunua HTC, jana HTC imetangaza kuwa Google imenunua vipaji kutoka kwenye kampuni hiyo kwa thamani ya dola za kimarekani zaidi ya bilioni 1.1. Wafanyakazi wapatao 2000 wengi kati ya wafanyakazi wa HTC wanaohamia Google ni ma injinia na madesigner ambao tayari walihusika kutengeneza simu za Pixel na wanaendelea kutengeneza toleo jipya.

Makamu wa Raisi anaehusika na hardware Rick Osterloh, jana alisema:

HTC IMEKUWA MSHIRIKA WA MUDA MREFU NA IMETENGENEZA MOJA YA SIMU ZA KUVUTIA ZA KIWANGO CHA JUU KWENYE SOKO. TUNAFURAHI KUIKARIBISHA TIMU YA HTC KUJIUNGA NASI KATIKA SAFARI HII

Google na HTC wamekuwa wakifanya kazi pamoja kwa miaka kadhaa sasa na pamoja wameweza kutengeza simu ikiwemo simu ya Android ya kwanza kabisa HTC Dream, Nexus One iliyotoka 2010, tableti ya Nexus 9 iliyotoka 2014, na simu ya Pixel ya mwanzo kabisa iliyotoka mwaka jana.

google htc deal
Makamu wa raisi wa hardware wa Google Rick Osterloh(kushto) akishikana mkono na CEO wa HTC Cher Wang (katikati). Taipei, Taiwan Septemba 21, 2017. REUTERS/Tyrone Siu

Kufuatia dili hili, HTC wataendelea kutengeza simu pia vifaa vya Virtual reality. Pia Google wamenunua baadhi ya haki miliki za HTC, na kampuni hizo mbili zimeingia makubaliano ya kushirikiana zaidi katika siku za usoni.

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive