Google yapigwa faini ya euro bilioni 4.34 na Umoja wa Ulaya

Kamisheni ya Umoja wa Ulaya kupitia kamishna wa ushindani bibi Margrethe Vestager, wametangaza kuipiga faini ya takribani Euro bilioni 4.3 kampuni ya Google kwa njia zake zisizofaa katika kuwanyamazisha wapinzani wake kupitia mfumo endeshi wake wa Android kwa kulazimisha kutumia injini ya utafutaji ya Google (Google Search).

Kamishna wa ushindani wa Umoja wa Ulaya, Bi. Margrethe Vestager akifafanua jambo kwenye mkutano na waandishi katika makao makuu ya umoja wa ulaya Brussels tarehe 18 mwezi julai, 2018

Habari kuhusu faini hii ambayo itakuwa ya kwanza kuwa faini kubwa kabisa kutolewa na Kamisheni ya Ulaya ilitangazwa kupitia mtandao wa twitter kwenye akaunti ya Kamishna Margrethe Vestager, pamoja na faini hii pia amsema Google imejiongezea umaarufu na ushikaji wa soko kwa kutumia njia zisizo halali kwa kuzuia makampuni mengine kuja na mbadala wa Google kama injini ya kutafutia.

Usikose Kusoma:  Cryptocurrency ni nini?

Moja ya uvunjaji wa sheria ambao kamishna ameuzungumza ni ule wa kampuni ya Google kuwalipa makampuni watengenezaji wakubwa wa simu za mkononi na vifaa vingine vinavyotumia mfumo endeshi wa Android ili vifaa hivyo viwe na app za Google search na Chrome. Kamishna akasisitiza kuwa njia hii sio halali.

Kampuni ya Google italazimika kulipa faini hiyo ambayo ni takribani asilimia 40 ya faida yake kwa mwaka 2017, na itatakiwa kubadili mbinu zake ili isiingie katika matatizo ya kupigwa faini zingine siku za usoni,  Kamisheni ya Ulaya ilisema

Usikose Kusoma:  Unataka kufanya mazungumzo ya kibinafsi katika mkusanyiko wa watu wengi?

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa