Hisa za Facebook zaporomoka baada ya kashfa ya kutumia taarifa za watumiaji bila ruhusa yao

Hisa za Facebook zimeporomoka kwa asilimia 6 ambazo ni sawa na takribani dola za kimarekani bilioni 30 baada ya kuibuka kwa taarifa za uchunguzi kuhusu kampuni ya Cambridge Analytica, kutumia taarifa za watumiaji zaidi ya milioni 50 bila idhini yao, taarifa hizo zilitumika kwenye kampeni ya urais ya Donald Trump aliyewatumia Cambridge Analytica kwa ajili ya matangazo yake ya kampeni kwa wapiga kura wa Marekani.

Usikose Kusoma:  Tigo, Selcom na Mastercard waungana kuleta huduma ya Masterpass QR nchini Tanzania

Watengeneza sheria wa Umoja wa ulaya siku ya jumatatu walisema wanafanya uchunguzi juu ya kampuni iyo inayotuhumiwa kuvuna taarifa za watumiaji wa facebook zaidi milioni 50 bila ruhusa yao.

Ripoti kutoka magazeti ya The New York Times, The Observer zinasema kampuni iyo ilikiuka sheria za Facebook kwa kuvuna taarifa za watumiaji kwa ajili ya utafiti. Tayari mashirika kadhaa yameshaanza utafiti juu ya kashfa hiyo.

Habari hii ya matumizi ya taarifa za wasomaji ilianza kuonekana kwenye gazeti la The Observer la Uingereza na The New York Times, ilitolewa na mvujishaji taarifa Christopher Wylie ambaye aliweka wazi namna Cambridge Analytica walivyoweza kuvuna na kutumia taarifa za watumiaji.

Usikose Kusoma:  Kashfa ya Cambridge Analytica yafanya Facebook kuzindua programu kusafisha mipangilio yako ya faragha.

Mwaka 2014 taarifa zilivunwa na Cambridge Analytica, kupitia mtafiti wa nje, waliwalipa hela kidogo watumiaji ili waweze kujibu maswali na kudownload app ambayo iliweza kuchukua taarifa binafsi za watumiaji hao kutoka kwenye majalada yao na taarifa kutoka kwa marafiki zao.

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa