Microsoft yathibitisha kuinunua GitHub kwa dola billioni 7.5

Baada ya tetesi kuvuma kwa majuma kadhaa, leo Microsoft wamethibitisha inainunua GitHub kwa gharama ya dola za kimarekani bilioni 7.5. Ripoti zilizoanza kuonekana juma lililopita zilisema Microsoft iko kwenye mazungumzo ya kuinunua maktaba hii kubwa inayotumiwa na wabunifu mbalimbali wa program duniani.

GitHub ni mtandao wenye maktaba zilizo wazi kutumiwa na kuboreshwa na watu wengine (Open Source libraries). Ilizinduliwa mwaka 2008 huko San Francisco Marekani. Makampuni mengi makubwa kwa madogo, taasisi za kiserkali na binafsi zimekuwa zikiweka code zao kwa ushirikiano na ma developer wengine duniani kote.

Usikose Kusoma:  Intel yaungana na Microsoft, HP, Dell, na Lenovo ili kuleta Chip za Laptops za 5G mwaka 2019

Tangu Satya Nadella awe CEO wa Microsoft, kampuni imebadilisha muelekeo na kukumbatia open source tofauti na miaka kumi iliyopita ambapo ilijulikana kwa kutaka kukandamiza Linux.

Siku za hivi karibuni Microsoft waliachia code za program zake kama PowerShell, Visual Studio Code, na Microsoft Edge JavaScript engine kwenye open-source, na zimekuwa hosted kwenye GitHub kwa watumiaji wengine kuzitumia na kuziboresha. Pia Microsoft imefanya kazi na Canonical (kampuni nyuma ya Ubuntu) ili kuileta Ubuntu kwenye Windows 10, pia wameinunua Xamarin kuwasaidia watengenezaji wa app za simu za mkononi.

Usikose Kusoma:  LG waonesha TV kubwa zaidi duniani yenye teknolojia ya 8K

Tayari kumeanza kuwa na sintofahamu kwa watumiaji wa GitHub kutoipenda Microsoft kutokana na historia yake ya kukandamiza uhuru wa kutumia code bure. Itabidi Microsoft walichukulie kwa umakini mkubwa jambo hili, maana tayari kampuni pinzani ya GitLab imeonesha ongezeko kubwa la watumiaji mara kumi zaidi kila siku wakiweka code zao huko.

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa