Nokia 6 (2018) yatangazwa

Jana kulivuja taarifa kwenye mitandao kuhusu simu ya Nokia 6 (2018). Basi leo kupitia tovuti yao, Nokia wametangaza rasmi kutoka kwa Nokia 6 (2018).

Jina halisi la simu hii ni Nokia 6 (second generation) na inaonesha itakuwa na karibu sifa nyingi za mtangulizi wake aliyetoka mwaka jana Nokia 6 (2017). Simu hii inakuja na mfumo endeshi Android Nougat ambapo inaweza kupandishwa hadhi mpaka Android Oreo.

  
Simu hii inakuja na chip ya Qualcomm Snapdragon 630 (mtangulizi wake alikuja na Snapdragon 430) pia inakuja na teknolojia ya kurekodi sauti ya OZO, na itakuwa na Bothie photo mode kwenye upande wa kamera.
Unaweza kuoda simu yako mapema hata kabla haijatoka kuanzia leo, ambapo simu yenye ukubwa 32GB itauzwa kwa dola za kimarekani 230 wakati yenye 64GB itaenda kwa dola za kimarekani 245, na simu itaanza kupatikana kuanzia mwezi wa kwanza mnamo tarehe 10. Tutegemee kuiona simu hii kwenye maonesho ya CES 2018 yanayoanza wiki ijayo.

Uchambuzi wa simu hii utaupata kwenye kipengele cha uchambuzi

Usikose Kusoma:  Wireless Storage: Njia rahisi ya kuhamisha Data kwenye simu yako ya android.

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa