Royole FlexPai : Simu ya kwanza inayojikunja bado ina safari ndefu

Simu hii ya aina ya kipekee ya kwanza kabisa duniani inayokunjika yenye kutumia mfumo endeshi wa Android, ilitangazwa mwishoni mwa mwaka 2018 huko china. Simu hii imeoneshwa kwa mara kwanza kwenye maonesho ya CES 2019 na kuvutia watu wengi.

Hata hivyo watu wengi walioijaribu simu hiyo wamesikitishwa na “kuharakishwa” kwa simu hiyo, imaana imekuwa chini ya matarajio ya wengi. Kitu pekee kilichokuwa cha kuvutia na cha kitofauti ni uwezo wa kukunjika, huku nynja zingine ikishindwa vibaya.

Simu hii ya Royole FlexPai itaanza kuuzwa nchini China kwa Yuan ya China 9,000 ambayo ni sawa na shilingi za kitanzania takribani 2,972,000 bila kodi.

flexpai-1-4-1220x813

 

Pande mbili za Royole FlexPai zimeunganishwa kiunganishi cha raba katikatiki, ambapo inapofunguliwa inakuwa na kioo chenye ukubwa wa inchi 7.8 na muonekano wa kuvutia zaidi kuliko inapofungwa na kuwa na vioo viwili vyenye ukubwa wa inchi kila kimoja ambapo inakuwa nene zaidi na muonekano usiovutia.

Usikose Kusoma:  Samsung Max: Programu mpya ya Android ya usimamizi na ufuatiliaji wa matumizi ya data.

flexpai-1-1-1220x813-1

Watengenezaji wa simu hii waliweka maanani swala la uimara wa simu hii kwa kuhakikisha kuwa inaweza vumilia mikunjo zaidi ya laki mbili 200,000 ambayo ni sawa na miaka kadhaa.

Simu ina line mbili na inapofungwa unaweza kutumia pande zote kama simu mbili tofauti na mfumo wa simu hii unaweza kugundua unatumia upande upi ili kuufanya kuwa upande mkuu.

flexpai-1-3-1220x813

Simu ina betri yenye uwezo wa 3970mAh, ina port ya USB-C na fingerprint scanner. Haina sehemu ya kuchomeka headphone na ikamera mbili nyuma zenye 16mp na 20mp. Kioo chake ni AMOLED chenye resolution ya 1920 x 1440.

Usikose Kusoma:  Tigo, Selcom na Mastercard waungana kuleta huduma ya Masterpass QR nchini Tanzania

Simu hii inakuja na  prosesa ya Snapdragon 855 ambayo ina uwezo mkubwa sana wa kufanya kazi mbalimbali pale unapokuwa simu na pale inapokuwa tablet. Iakuja na RAM ya GB 6 pamoja na hifadhi ya ndani GB 128, pia inakuja na machaguo mengine ya RAM ya GB 8 na hifadhi ya GB 256 na toleo linakuja na RAM ya GB 8 na hifadhi ya GB 512.

flexpai-1-2-1220x813

Mfumo endeshi wa Android 9 Pie kwenye simu hii umeonekana kushindwa kufanya kazi vizuri hasa simu inapokunjuliwa ama kugeuzwa kutoka landscape mode au portrait mode.

hitimisho

Tunaipongeza kampuni iliyo nyuma ya simu hii ya FlexPai kwa kuwa ya kwanza kuja na simu ya kitofauti na kipekee inayojikunja. Ila imezindua mapema kuliko kawaida tena itauzwa kwa gharama kubwa kupita kiasi kwa simu ambayo ni toleo la kwanza .

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa