Safaricom iko mbioni kupeleka huduma ya M-Pesa nchini Ethiopia

Kwa mujibu wa taarifa ambayo imeanza kuonekana kwenye tovuti ya shirika maarufu la habari ya Reuters inasema kampuni kubwa kabisa ya mawasiliano nchini Kenya iko katika hatua nzuri ili kuanza kutoa huduma ya M-Pesa nchini Ethiopia. Hatua hii inaifanya huduma hii ambayo tayari ni maarufu Afrika mashariki hasa Kenya na Tanzania kuzidi kujitawanya sehemu zingine zaidi.

Usikose Kusoma:  Jaribu Hii kuongeza Speed ya Computer yako ya zamani.

Chanzo cha habari hii kinasema kuwa Vodafone Uingereza ambayo ndio kampuni mama ya Safaricom, itatoa leseni ya M-Pesa kwa kampuni kubwa kabisa nchini Ethiopia ya Ethio Telecom wakati wao Safaricom watakuwa kuwa waki host server za M-Pesa kutoka Nairobi.

Chanzo kimeiambia Reuters kuwa Safaricom itapokea asilimia 25 ya mapato yatokanayo na huduma ya M-Pesa kwa kuanzia na asilimia hizo zinatarjiwa kushuka mpaka 10 kadri huduma inapozidi kukua.

Usikose Kusoma:  Nokia 9 PureView yenye kamera tano yazinduliwa kwenye maonesho ya MWC 2019

Huduma ya M-Pesa imekuwepo nchini Kenya tangu mwaka 2007 na imekuwa ikikukua kwa kasi ambapo mpaka sasa ina watumiaji zaidi ya milioni 23 kwa Kenya pekee, na watumiaji zaidi milioni 30 katika nchi zingine zaidi ya 10.

Pamoja na Safaricom, makampuni mengine ambayo yameonesha nia ya kuwekeza nchini Ethiopia ambayo ina takribani wananchi milioni 100, ni pamoja na benki ya KCB Group.

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa