WhatsApp kudhibiti idadi ya message za kuforward ili kuzuia usambazaji habari za uzushi

Ni baada ya kulaumiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa usambazaji wa habari za uzushi na hatari huko India

Ni chini ya majuma mawili yamepita tangu WhatsApp watangaze kuongeza alama kwenye jumbe zinazosambazwa “forwarded message”, leo wametangaza kufanya maboresho mahususi kwa ajili ya kukabiliana na usambazaji wa taarifa hatari na zisizo sahihi huko India.

Alhamisi hii wametangaza majaribio ya kudhibiti usambazaji wa jumbe kupitia WhatsApp, ambazo mara nyingi huwa ni si za kweli au za kupotosha. Kuanzia sasa watuniaji wataweza kusambaza jumbe 20 tu kwa wakati mmoja, kampuni hiyo inaamini kwa namna hiyo itawapungizisha kasi wanaopenda kusambaza jumbe hizo kila mara.

Usikose Kusoma:  Ifahamu simu ya Samsung Galaxy Note 8

Kwa India, watumiaji wataweza kusambaza jumbe 5 tu mara moja. Katazo hili litasababisha kufungiwa kwa akaunti itakayosambaza ujumbe mmoja zaidi ya mara 5 na kusambabisha akaunti hiyo kukosa uwezo wa sambaza (kuforward) jumbe kwa muda. Kabla ya utaratibu huu mpya, watumiaji walikuwa wanaweza kusambaza jumbe mpaka 250 kwa mara moja.

Katika chapisho kwenye blog ya WhatsApp imeonesha kuwa watumiaji wa India wanasambaza jumbe, picha na video kwa wingi kupita nchi nyingine yoyote duniani. India yenye watumiaji wa WhatsApp takribani milioni 250 ndio inayoongoza kwa watumiaji wengi. Katazo hili kuhusu usambazaji wa taarifa kupitia WhatsApp linakuja baada ya kutokea ripoti za ugomvi mkubwa huko India uliosababishwa na usambazaji wa taarifa feki.

Usikose Kusoma:  Kufa kwa symbian neema kwa asha sasa yapata multitasking na swipe ui

WhatsApp inaendelea kuboresha huduma zake kuongeza vitu vipya kila inapohitajika, mpaka sasa wameweka alama ya “forwarded message” kwenye jumbe zinazosambazwa ili kumtahadharisha mpokeaji kuwa ujumbe haukuandikwa na mtumaji, lengo likiwa ni kuwafanya watumiaji kuwa makini na jumbe za namna hiyo.

 

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa