Hakuna tena majina ya vyakula, toleo jipya la Android litaitwa Android 10

Android  Q ndio jina lilikuwa linafuata kwa toleo jipya la mfumo endeshi wa simu janja na tableti wa Android. Google wameamua kuachana na mfumo wa kuyapa matoleo ya Android majina ya vyakula (desserts) kama ambavyo walifanya kwa matoleo yaliyopita, na badala yake wameanza kuweka herufi, na kwa kuanzia wameita toleo jipya Android 10. Kwa miaka zaidi ya 10 sasa Google wamekuwa wakitumia majina ya vyakula yakifauatana kwa alphabet kuanzia toleo la 1.5, ambapo waliyapa majina kama;

 • Android 1.5 Cupcake
 • Android 1.6 Donut
 • Android 2.0/2.1 Éclair
 • Android 2.2 Froyo
 • Android 2.3 Gingerbread
 • Android 3.0/3.1/3.2 Honeycomb
 • Android 4.0 Ice Cream Sandwich
 • Android 4.1/4.2/4.3 Jelly Bean
 • Android 4.4 KitKat
 • Android 5.0/5.1 Lollipop
 • Android 6.0 Marshmallow
 • Android 7.0/7.1 Nougat
 • Android 8.0/8.1 Oreo
 • Android 9.0 Pie

Mabadiliko haya yanakuja baada ya mrejesho kutoka kwa watumiaji wa mfumo endeshi huu wa Android kuonesha kukanganywa na majina haya, hasa kwa watumiaji wa nchi ambazo hawafuati utaratibu wa majina kwa mfumo wa alfabeti.

Pamoja na kubadili mfumo wa majina, Google pia wameamua kufanyia mabadiliko logo ya Android, hayo yalitangazwa na Aude Gandon, ambae ni director wa Android, muonekano utakuwa na maandishi yenye “muonekano wa kisasa”. Pia kutakuwa na uso wa roboti ya kijani ya Android. Mabadiliko mengine yaliyofanywa katika logo ni rangi zitakazotumika kwenye logo hasa kwenye maandishi kutoka kijani na kuwa meusi.

Katika chapisho kwenye makala ya blogu ya Google, imesema mabadiliko haya yataanza kuonekana rasmi majuma machache yajayo toleo jipya litakapozinduliwa rasmi.

Endelea kufuatilia Mtaawasaba kwneye mitandao ya kijamii ili uwe wa kwanza kupata taarifa kila Zinapotufikia

WAWEZA SOMA:  Samsung Galaxy S9: kuzinduliwa Februari 25

 

HAKUNA MAONI

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa