Huawei wazindua HarmonyOS, mfumo endeshi kwa ajili ya vifaa janja

Katika siku ya kwanza ya mkutano mkubwa wa madeveloper unaofanywa na Huawei kwa jina la Huawei Developer Conference, unaoendelea huko Dongguan City, mfumo endeshi uliopewa jina la Harmony Os, ambao utakuwa mbadala wa Android umezinduliwa. Mfumo endeshi huu unasemekana kuwa na kasi na rahisi kutumia kuliko Android.

Mfumo endeshi huu utaanza kutumika kwenye vifaa kama Televisheni, na miaka mitatu baadae utatumika kuendesha vifaa vingine vikiwemo saa janja na hata kwenye magari.

Mkurugenzi mtendaji wa Huawei alisema Harmony Os utakuwa ni mbadala wa Android kwenye simu janja zao pindi itakapotokea wakazuiwa tena kutumia Android (kama ilivotokea hivi karibuni).

“Kama hatutaweza kutumia Android siku zijazo , basi tutahamia kwenye Harmony OS mara moja” mkurugenzi huyo aliwafafanulia wahudhuriaji wa mkutano huo, huku akisisitiza kuwa kuhama Android sio vigumu kiivyo.

Bidhaa ya kwanza kabisa kutumia mfumo endeshi huu itakuwa ni Honor Vision TV set, ambayo itazinduliwa kesho huko China.

Taarifa za mfumo endeshi mpya kutoka Huawei zilianza kusikika mapema baada zuio la marekani kufanya biashara na makampuni ya China ikiwemo Huawei mwezi wa Tano mwaka huu, hata hivyo baadae Marekani waliruhusu Huawei kufanya kazi na makampuni ya Marekani.

Ili kuvutia wabunifu zaidi, Huawei wameruhusu mfumo endeshi huu ambao unamuwezesha mtumiaji kutumia app za android, kupatikana bure na inaruhusiwa kuufanyia maboresho. Hata hivyo kwa sasa Huawei wanajaribu kuhakikisha mfumo huu unakuwa na nguvu kushika soko la China, lengo hili likitimia ndio wataanza kuweka mkazo kwenye soko la dunia nzima.

Endelea kuwa nasi tuendelee kukupa taarifa zaidi kuhusu mfumo endeshi huu na habari zingine nyingi za teknolojia.

WAWEZA SOMA:  Huu ndio muonekano wa Samsung Galaxy S10

 

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa