Huu ndio muonekano wa Samsung Galaxy S10

Zikiwa zimebaki siku kadhaa  kabla Samsung hawajangaza simu zao mpya (kawaida uwa wanazindua mwezi wa pili mwishoni), tayari mvujishaji maarufu Evan Blass ameachia picha ya kwanza yenye muonekano halisi wa simu ya Samsung Galaxy S10. Muonekano wa simu hii ni tofauti na picha mbalimbali zilizokuwa zikiibuka siku zilizopita zikijaribu kubashiri muonekano wa simu hii mpya.

Katika picha hii iliyoachiwa inaonesha muonekano wa simu hii pamoja na kamera iliyopachikwa chini ya kioo kilichopewa jina la Infinity-O Display ikiwa ni jitihada za kampuni ya Samsung kukwepa kuweka notch kwenye simu zake, trend ambayo ilianzishwa na kampuni ya Apple kwenye simu za iPhone na kufuatwa na watengenezaji karibu wote wa simu za Android.

Taarifa za awali zinadai simu mpya ya Galaxy S10 itakuja ikiwa na matoleo matatu tofauti, ambayo yatatofautiana kwa ukubwa wa kioo. Toleo lenye kioo chenye ukubwa wa inchi 5.8 ndio linatarajiwa kuwa la wastani likiwa na kioo kilichonyooka badala kioo kilichojikunja kama itakavokuwa kwenye matoleo mengine, matoleo mengine yatakuja na vioo vilivojikunja vyenye ukubwa inchi 6.1 na 6.4.

Kwa muonekano wa picha iliyovujishwa na Evan Blass kwenye mtandao wa twitter inawezekana ni toleo la Galaxy S10 lenye kioo chenye ukubwa wa inchi 6.1 na kamera ya mbele iliyo chini ya kioo iliyokaa upande wa kulia juu, tofauti na simu ya Samsung A8s ambayo ndio ya kwanza kutumia kioo cha Infinity-O Display, kamera yake ya mbele iko upande wa kushoto.

Katika tweet yake Evan Blass ameongeza kuwa, pamoja na sifa zingine nyingi, simu hizi zitakuwa na uwezo wa kuchaji simu na saa janja zingine bila kuunganisha waya. Toleo kubwa ambalo ndio litakuwa la bei ghali linasemekana kuwa na uwezo wa teknolojia ya 5G.

WAWEZA SOMA:  Njia rahisi ya kuzuia Automatic Updates za Windows 10

Endelea kupitia tovuti yako pendwa ya mtaawasaba ili upate kujua taarifa za simu hii kadri zitakavokuwa zikitufikia. usisahaua kutufuata kwenye mitandao ya kijamii, na ku subscribe kwenye channel yetu ya youtube @mtaawasaba

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa