Instagram iko mbioni kuachia Direct Messages kwa watumiaji wa kompyuta

Instagram iko kwenye majaribio ya kuwezesha watumiaji wa kompyuta kutuma na kupokea jumbe kupitia mtandao maarufu kama Direct Messages, hii ni kwa watumiaji wa vivinjari vya kompyuta na vivinjari vya simu janja. Kwa mujibu wa tweet iliyochapishwa na mtafiti Jane Manchun Wong, ambae ameonesha picha ya muonekano wa DM kwenye kompyuta. Taarifa hizi zilianza kuchapishwa na mtandao wa TechCrunch, ambapo kwa mujibu wa mtandao huo, Instagram imethibitisha mpango huo japo hawajaanza kufanya majaribio kwa watu wengi.

Katika muonekano wa sasa, huduma nyingi zinazopatikana kwenye app hazipatikani kwa watumiaji wa vivinjari, huduma kama Direct Message, kupandisha picha na huduma zingine ambazo zinapatikana kwenye app. Huduma hii itakuwa ni hatua kubwa kwa Instagram katika kuwabakiza watumiaji wa kompyuta wasiotumia app.

Habari hii imekuja siku si nyingi baada ya kampuni mama ya Facebook kutangaza mpango wake wa kuunganisha huduma za kutuma jumbe kati ya Facebook Messenger, Instagram DM na WhatsApp. Sababu nyingine inayodhaniwa kusababisha kufikia hatua hii ni, majaribio ya app iitwayo Direct iliyoanza kufanyiwa majaribio tangu mwaka 2017 katika nchi zipatazo sita. App hiyo ambayo itakuwa ni ya kujitegemea katika kutuma na kupokea jumbe za Instagram, inasemekana ni moja ya hatua ya kuunganisha huduma.

Kwa sasa Facebook imetoa fursa kwa wafanyabiashara wa Marekanina Brazil kuweza kujibu jumbe za Instagram Direct Messages kutoka moja kwa moja kwenye Facebook Messenger, hii ikiwa ni hatua ya mwanzo kuunganisha huduma hizo bila kujali anaetuma anatumia kivinjari ama anatumia app, kutoka kwenye kompyuta ama simu ya mkononi.

 

WAWEZA SOMA:  Sharp wazindua simu janja ya kwanza yenye notch mbili

Maoni 1

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa