Jinsi ya kudownload na ku install iOS 15 kwenye simu yako ya iPhone

Alexander Nkwabi 2 190
Apple leo wameachia sasisho kubwa la mfumo endeshi wa iOS 15 kwa ajili ya simu za iPhone.

Sashisho hili ni bure kabisa kushusha na linazihusu simu zote kuanzia iPhone 6s na kuendelea, vizazi vyote vya iPhone SE pia vitapata sashisho hili bila kusahau toleo jipya la ipod touch. Kwa watumiaji wa iPad wao watapata iPadOs 15 na wale wa Apple watch watapata watchOS 8 leoleo pia.

Hapa chini tunakufafanulia namna ya kuinstall iOS 15 kwenye simu yako ya iPhone, na maelekezo haya pia yanafanana kwenye iPadOS kwa watumiaji wa iPad. Kabla ya yote hakikisha kifaa chako kina uwezo wa kudownload sasisho hili.

Simu gani zitapata iOS 15 au iPadOS 15?

iPhone 12 MiniiPad Pro 12.9-inch (kizazi cha 5)
iPhone 12iPad Pro 11-inch (kizazi cha 3)
iPhone 12 ProiPad Pro 12.9-inch (kizazi cha 4)
iPhone 12 Pro MaxiPad Pro 11-inch (kizazi cha 2)
Phone 11iPad Pro 12.9-inch (kizazi cha 3)
iPhone 11 ProiPad Pro 11-inch (kizazi cha 1)
iPhone 11 Pro MaxiPad Pro 12.9-inch (kizazi cha 2)
iPhone XSiPad Pro 12.9-inch (kizazi cha 1)
iPhone XS MaxiPad Pro 10.5-inch
iPhone XRiPad Pro 9.7-inch
iPhone XiPad (kizazi cha 8)
iPhone 8iPad (kizazi cha 7)
iPhone 8 PlusiPad (kizazi cha 6)
iPhone 7iPad (kizazi cha 5)
iPhone 7 PlusiPad Mini (kizazi cha 5)
iPhone 6siPad Mini 4
iPhone 6s PlusiPad Air (kizazi cha 4)
iPhone SE (kizazi cha 1)iPad Air (kizazi cha 3)
iPhone SE (kizazi cha 2)iPad Air 2
iPod Touch (kizazi cha 7)

 

Jinsi ya install iOS 15 na iPadOS 15

Kabla hujaanza zoezi hili hakikisha simu yako ina chaji ya kutosha, pia hakikisha una data ya kutosha au una chanzo kingine kama Wi-Fi ili kukuharakishia na kukurahisishia mchakato.

Kama kila kitu kiko sawa basi fata hatua zifuatazo;

1. nenda Settings app.

2. halafu chagua General.

3. kisha bofya Software Update. 

4. Kwenye kipengele cha Also Available, bofya Upgrade to iOS 15.

5. Chagua Download and install ili kuruhusu mchakato wa ku install kuanza. Unaweza ombwa kuingiza passcode kama unayo.

Fuata maelekezo ili kukamilisha mchakato wa kuinstall. Simu ikimaliza ilo zoezi itajizima kisha kujiwasha. itakapowaka itakuwa na iOS 15. Hatua ni hizi hizi kufuata kama unatumia iPad na unataka kuipa iPadOS 15.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unatembelea tovuti ya Mtaawasaba kila siku, pia usisahau kujiunga nasi kupitia channel yetu ya Mtaawasaba kupitia YouTube.

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
2
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive