Kutana na Kiatu Janja kwa ajili ya wazee

Mwandishi Diana Benedict

Teknolojia ya vifaa janja vinavovaliwa (wearables) inazidi kukua kila kukicha. Mwaka huu katika maonesho ya CES 2018 yanayoanza rasmi leo tarehe 8 mwezi wa kwanza 2018, kampuni ya kifaransa ya E-Vone inakuja na viatu janja (smart shoes) maalumu kwa watu wenye umri mkubwa, wafanyakazi na wanaosafiri safiri, ambapo viko katika muundo wa Sneaker, viatu vya kutembelea(hiking) na viatu vya kazi.

evone smart shoes 1

Ndani ya viatu ivi kuna sensa kadhaa ambazo zimewekwa katikati ya sole ya kiatu, ambazo ni GPS, accelerometer, gyroscope na mfumo wa presha unaotambua pale mtu anapovaa kiatu. Msemaji wa E-Vone alitanabaisha kuwa viatu ivyo havihitaji kuwa paired na simu kwa maana vinakusanya taarifa vyenyewe. , viati hivyo vyenye mfumo ya GSM ndani yake, GPS na antena za LoRa ambapo kama kutatokea lolote lisilo la kawaida vitatuma taarifa kwenye namba ya mtu atakaepokea ujumbe wakati wa dharura.

Viatu hivyo havijaanza kuuzwa, kwa sasa haijulikani ni lini vitaanza kupatikana wala bei zake

Mwandishi Diana Benedict Mwandishi
Mitandao ya Kijamii
Diana Benedict. Digital Creator | IT Specialist | Graphics Designer | Web Designer | Web SEO | Contents Management | UI/UX Designer and Social Media Management.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive