Kila kitu unachotakiwa kujua kuhusu Samsung Galaxy S10, S10 Plus, S10e, na S10 5G

Baada ya picha nyingi zilizovuja kuhusu simu mpya zitakazopeperusha bendera ya Galaxy kwa mwaka huu, hatimaye Samsung ikisherehekea miaka kumi tangu simu ya kwanza ya Galaxy itoke, wazindua rasmi simu tatu zitakazokuwa kwenye familia ya Galaxy S kwa mwaka huu, ambazo ni Galaxy S10, the S10 plus na S10e kwenye tukio la uzinduzi maarufu kama Samsung Unpack leo Februari 20, 2019. Simu zote zikitamba kwa teknolojia ya kamera ya mbele iliyopenyezwa kwenye tundu ndani ya kioo cha mbele.

Samsung hawakuishia hapo,bali pia waliachia matoleo mengine ya Galaxy S10 moja ikiwa ni Performance edition na ingine 5G edition (ambayo haitatoka kwenye nchi nyingi kwa kutokuwa na teknolojia ya 5G bado). Hizi simu zote zinatarajiwa kuingia sokoni mnamo tarehe 8 mwezi wa tatu 2019, tayari unaweza kuagiza simu yako kupitia maduka ya tiGO Tanzania na maduka ya Samsung.

Hebu tuzipitie simu zote zilizozinduliwa huku tukizilinganisha na kuzitofautisha

Muundo

Simu zote za familia ya Galaxy S10 zinafanana kimuonekano kwa nje. Upande wa mbele zote zina kioo kilichojikunja (isipokuwa S10e kioo chake ni bapa) kutoka upande mmoja na upande mwingine ambacho ni kigumu maarufu kama  Gorilla Glass 6. Simu zote zina uwezo wa kutoingia maji kwa muda wa nusu saa kwenye kina cha mita moja na nusu.

Simu zote kwa upande wa juu na chini zina bezel na kidevu kidogo sana, zina iris scanner kama ilivokuwa utamaduni wa Galaxy S na Note tangu 2016. Simu hizi zina kamera ya mbele iliyopachikwa ndani ya shimo lilitobolewa kiufundi chini ya kioo, Samsung wameupa jina muundo huo kama “Infinity-O,” ambao tulianza kuuona kwenye simu za Galaxy A8 zilizotoka mwezi wa kwanza. Kwa simu za S10 na S10e zina kamera moja ya mbele, wakati S10+ ina kamera mbili upande wa mbele.

Hapa chini ni ukubwa wa vioo na resolution zake:

 • Galaxy S10e: 5.8 inches, 3040 x 1440 pixels (522 PPI)
 • Galaxy S10: 6.1 inches, 3040 by 1440 pixels (550 PPI)
 • Galaxy S10+: 6.4 inches, 2280 by 1080 pixels (522 PPI)

Galaxy S10 vioo vye uwezo wa kuona picha angavu za HDR, hii inawezeshwa na kioo cha AMOLED. Samsung wametamba kuwa kwa teknolojia ya kioo cha Dynamic AMOLED unaweza kuona rangi milioni 16.

Samsung Galaxy S10 na S10+ zina sensa ya ultrasonic ya kufungua simu kwa kutumia kidole, teknolojia hii ya ultrasonic fingerprint sensor imesambazwa na kampuni ya Qualcomm na iko chini ya kioo cha mbele. Samsung wanadai simu hizi zinafunguka haraka kuliko wapinzani wao OnePlus 6T, Vivo Nex, na Xiaomi Mi 8 ambao wameanza kuitumia teknolojia hii, S10e yenye ina fingerprint scanner ya kawaida.

WAWEZA SOMA:  Jinsi ya kuangalia video za youtube na subtitle

S10 na S10+ zina kamera tatu na flash upande ywa nyuma sawasawa na simu kama LG V40 au huawei Mate 20 pro, wakati kwa upande S10e kuna kamera mbili tu. upande wa chini kuna sehemu ya kuchajia simu ya USB Type-C, sehemu ya kuchomeka headphone na kuna loudspeaker. upande wa kushoto pembeni simu zote zina vitufe vya kuongeza na kupunguza sauti bila kusahau kitufe cha Bixby program ya usaidizi ambacho kinaweza badilishwa matumizi, upande wa kulia ni kitufe cha kuzima na kuwasha simu.

Mfumo endeshi

Simu zote zinakuja na mfumo endeshi wa Android 9 Pie ukiwa umefunikwa ngozi mpya kabisa kutoka Samsung ilibatizwa jina la One UI, ikiwa ni mbadala wa Samsung Experience na Touchwiz kwenye simu za matoleo ya awali.

Tupitie mifumo mbalimbali kwa upande wa software kwenye simu hizi.

OneUI

One UI ilianza kutumika kwenye simu za S9 na Note 9 miezi michache iliyopita ikiwa ni mbadala wa Samsung Experience

Pamoja na maboresho mengine mengi yaliyofanywa kwenye mfumo huu, maboresho makubwa yaliyofanywa katika One UI ni kusogeza vitu vyote vinavyotumika mara kwa mara upande wa chini wa simu ili kumrahisihia mtumiaji anatumia simu zenye urefu mkubwa kama hizi zilizozinduliwa leo.

Pia kuongezwa kwa dark mode kwa simu nzima inaleta hamasa hasa katika swala zima la kuokoa chaji na kufaidi kioo cha AMOLED.

Simu zote tatu zinakuja na app ya Adobe Premiere Rush, kwa ajili ya kuedit video kwenye simu, tablet ama kwenye kompyuta.

Bixby

Simu hizi pia zinakuja na app ya usaidizi kutoka Samsung maarufu kama Bixby, imekuwepo tangu enzi za S8 na Note8. Bixby inatumia teknolojia ya AI ili kuweza kuwasiliana na mtumiaji wa simu.

DeX

Kama ilivokuwa kwenye Note9, Sasa hivi utahitaji waya wa USB Type-C-to-HDMI ili uweze kufaidi DeX

 

Betri, RAM, hifadhi na muunganisho

Kutokana na mambo mengi zinazofanya simu hizi za familia ya Galaxy S10, zinakuja na betri zilizoshiba ili ziweze kukaa na chaji muda wa kutosha huku zikifanya majukumu yake kama inavyotakiwa.

ukubwa wa betri za simu hizi ni kama ifuatavyo:

 • Galaxy S10e: 3,100mAh
 • Galaxy S10: 3,400mAh
 • Galaxy S10+: 4,100mAh
WAWEZA SOMA:  Ripoti: Tanzania yafikisha watumiaji wa Intaneti milioni 23

Simu hizi zimeongezewa uwezo wa kuchaji vifaa vingine wirelessly kwa kutumia teknolojia walioipa jina la powershare. kwa hiyo unaweza kuchaji simu yako ingine ama galaxy bud zako haraka haraka.

simu zote tatu zina teknolojia ya PowerShare, japo ukubwa wa RAM zao haufanani. Hapo chini kuna ulinganifu wa RAM

 • Galaxy S10e: 6GB RAM, 128GB storage (expandable up to 512GB via microSD)
 • Galaxy S10: 8GB RAM, 128GB/512GB storage (expandable up to 512GB via microSD)
 • Galaxy S10+: 8GB RAM, 128GB/512GB storage (expandable up to 512GB via microSD)

Kuna toleo la Galaxy S10+ lenye RAM ya 12GB na hifadhi ya 1TB ambalo litatoka siku za baadae

Kamera na Spika

Kwa upande wa kamera Samsung uwa hawaangushi wapenzi wake, maana uwa wanakula sahani moja na ma heavy weight kama vile Google Pixel na iPhone, na safari hii Samsung wamepania kufunika kwenye upande huu kwa maboresho makubwa upande wa kamera

 

AKG

Simu zote tatu zinakuja uwezo wa kucheza kwa sauti ya stereo kupitia spika ya juu na loudspeaker upande wa chini. Zote zimechujwa kwa teknolojia ya AKG zikiwa na uwezo wa Direct Stream Digital (DSD) format (64/128) na Dolby’s Atmos 3D simulated surround sound kwa baadhi ya apps

Specs

  Mlinganisho wa simu za familia ya Galaxy S10  
SimuGalaxy S10eGalaxy S10Galaxy S10+Galaxy S10 5G
Mfumo endeshiAndroid 9 Pie
One UI 1.1
Android 9 Pie
One UI 1.1
Android 9 Pie
One UI 1.1
Android 9 Pie
One UI 1.1
Kioo5.8-inch AMOLED, 2280x1080 (19:9)6.1-inch AMOLED, 3040x1440 (19:9)6.4-inch AMOLED, 3040x1440 (19:9)6.7-inch AMOLED, 3040x1440 (19:9)
ProsesaSnapdragon 855
or Samsung Exynos 9820
Snapdragon 855
or Samsung Exynos 9820
Snapdragon 855
or Samsung Exynos 9820
Snapdragon 855
Hifadhi128/256GB128/512GB128GB/512GB/1TB256GB
Memori kadi?microSDmicroSDmicroSDNo
RAM6/8GB8GB8/12GB8GB
Kamera ya nyuma12MP Super Speed Dual Pixel, OIS, f/1.5 or f/2.412MP Super Speed Dual Pixel, OIS, f/1.5 or f/2.412MP Super Speed Dual Pixel, OIS, f/1.5 or f/2.412MP Super Speed Dual Pixel, OIS, f/1.5 or f/2.4
Kamera ya Nyuma ya TelephotoN/A12MP, OIS, f/2.412MP, OIS, f/2.412MP, OIS, f/2.4
Kamera ya nyuna ya Ultrawide16MP, f/2.216MP, f/2.216MP, f/2.216MP, f/2.2
Kamera ya mbele10MP, f/1.9, Dual Pixel AF10MP, f/1.9, Dual Pixel AF10MP, f/1.9, Dual Pixel AF10MP, f/1.9, Dual Pixel AF
MuunganishoWi-Fi 6, 2Gbps (Cat20) LTE, Bluetooth 5.0 LEWi-Fi 6, 2Gbps (Cat20) LTE, Bluetooth 5.0 LEWi-Fi 6, 2Gbps (Cat20) LTE, Bluetooth 5.0 LE5G NR, 2Gbps (Cat20) LTE, Wi-Fi 6 Bluetooth 5.0 LE
Teknolojia ya sautiStereo speakers
Dolby Atmos
3.5mm headphone
Stereo speakers
Dolby Atmos
3.5mm headphone
Stereo speakers
Dolby Atmos
3.5mm headphone
Stereo speakers
Dolby Atmos
3.5mm headphone
Betri3100mAh3400mAh4100mAh4500mAh
ChajiQuick Charge 2.0 (15W)
Fast Wireless Charging 2.0 (12W)
Quick Charge 2.0 (15W)
Fast Wireless Charging 2.0 (12W)
Quick Charge 2.0 (15W)
Fast Wireless Charging 2.0 (12W)
Super Fast Charge (25W)
Fast Wireless Charging 2.0 (12W)
Uwezo wa kutoingia majiIP68IP68IP68IP68
UlinziSide fingerprint sensor
Face recognition
Ultrasonic fingerprint sensor
Face recognition
Ultrasonic fingerprint sensor
Face recognition
Ultrasonic fingerprint sensor
Face recognition
Vipimo142.2 x 69.9 x 7.9mm
150 g
149.9 x 70.4 x 7.8mm
157 g
157.6 x 74.1 x 7.4mm
175 g (Ceramic: 198 g)
tbd
RangiFlamingo Pink, Prism Blue
Prism Black, Prism White, Prism Green (global)
Flamingo Pink, Prism Blue
Prism Black, Prism White, Prism Green (global)
Flamingo Pink, Prism Blue Prism Black
Prism White, Prism Green (global)
tbd
Bei$750$900$1000tbd
WAWEZA SOMA:  WhatsApp kudhibiti idadi ya message za kuforward ili kuzuia usambazaji habari za uzushi

Gharama na Neno la mwisho

Huu ndio mtiririko wa bei elekezi kwa Tanzania:

 • Samsung Galaxy S10 – Tsh 2,435,000/=
 • Samsung Galaxy S10e – Tsh 2,022,00/=
 • Samsung Galaxy S10 Plus – Tsh 2,715,000/= (GB 128) wakati toleo la GB 512 la Galaxy 10 Plus itakuwa ni Tsh 3,265,000/=

Kwa mujibu wa post ya instagram ya Samsung Tanzania, watu 100 wa kwanza kuagiza simu za Galaxy S10 au Galaxy S10e watapata na earphones za Galaxy buds bure zenye thamani ya Tsh 465,000/=.

Pia watu wa kwanza 50 kuagiza Galaxy S10 Plus watapata saa janja za Galaxy Sport yenye thamani ya Tsh 465,000/=.

Watumiaji wataweza kuagiza simu hizi kupitia maduka ya Tigo na yale ya Samsung sehemu yeyote nchini Tanzania.

Galaxy S10, Galaxy S10+, na Galaxy S10e zitapatikana kwa rangi nyeupe, nyeusi, bluu, and pink. Galaxy S10+ pia itapatikana rangi: ceramic black and ceramic white.

Endelea kutembelea ukurasa huu ili tuendelee kukujuza kila habari mpya itakapotufikia.

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa