kama lilivyo jina lake chromebook pixel ni laptop ambayo inakuja na kioo cha technolojia ya juu chenye resolution kubwa kupambana na laptop nyengine ambazo zipo vizuri maeneo hayo kama laptop za mac (laptop za apple). laptop hii si kama laptop tulizozizoea za windows au za apple, hii laptop inatumia operating system ya chrome. hii ni operating system inayofanya mambo yote online. lakini kikwazo kikubwa kwa hii laptop ni bei, inauzwa dola 1300 (zaidi ya million 2 za kitanzania) kwa wifi version au ukitaka yenye lte(4g) itafika dola 1500 kama milion 2 na nusu.