Mahakama Kenya Yazuia Baadhi ya Vifungu vya Sheria ya Makosa ya Mtandaoni

Mahakama kuu nchini Kenya imevizuia vifungu 26 vya Sheria mpya ya Matumizi Mabaya ya Kompyuta na Makosa ya Mtandao mpaka hapo shauri litakaposikilizwa, hatua hii inafikiwa baada vya chama cha Wanahabari na waendeshaji wa Blogu kufungua pingamizi.

Sheria hiyo ya Matumizi Mabaya ya Kompyuta na Makosa ya Mtandao iliyotiwa saini na Rais Uhuru Kenyatta wiki mbili zilizopita, inalenga kukabiliana na matumizi mabaya ya mtandaoni ambayo hayakujumuishwa katika sheria zinazohusianana mitandao ya kijamii.

Akitoa uamuzi huo Jaji wa Mahakama Kuu, Chacha Mwita amesema kuwa sheria hiyo ni kandamizi kwa haki za binadamu ikiwemo uhuru wa kujieleza. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 18 mwaka huu ambapo itasikilizwa tena.

Chama cha wamiliki mitandao nchini Kenya (Bloggers Association of Kenya) na chama cha waandishi wa habari cha Kenya (KUJ) walishinda mahakamani hatua za kuzuia sehemu zake kadhaa. Jumanne, jaji wa mahakama kuu, Chacha Mwita, aliorodhesha sehemu 26 za sheria hiyo kama kanuni ambazo zingeonyesha haki na uhuru wa msingi na kutoa amri za kumzuia yeyote anayeshitakiwa chini ya vifungu hivyo, wakati wa kusubiri uamuzi utakaotolewa Julai 18.

Mkurugenzi wa BAKE , James Wamathai, alisema: “Vifungu hivi vinadaiwa kudhibiti habari za uwongo lakini kwa bahati mbaya hii ni kinyume cha katiba… kuna sheria za kupunguza makali ya kesi wakati mtu anadanganya, hatutaki hali hii.”

Sehemu zingine za sheria zinatoa adhabu kwa ujasusi mtandaoni na picha au filamu za ngono zinazohusisha watoto.

Jaji Chacha Mwita ametangaza kwamba vifungu vifuatavyo vimesimamishwa hadi kesi itakaposikilizwa: Kifungu cha 5 – Muundo wa Kamati Taifa ya Uratibu wa Kompyuta na Makosa ya Mtandao

WAWEZA SOMA:  Viongozi wa makundi ya Whatsapp watakiwa kutoa taarifa za uhalifu

Kifungu cha 16 – Uingilizi usioruhusiwa

Kifungu cha 17- Ukwamishaji usioruhusiwa

Kifungu cha 22 – Machapisho ya uwongo Kifungu cha 23 – Uchapishaji wa habari za uwongo

Kifungu cha 24- Picha au filamu za ngono zinazohusu watoto

Kifungu cha 27 – Usumbufu wa makosa ya mtandao

Kifungu cha 28 – Kukaa na habari za makosa ya mtandao

Kifungu cha 29 – Wizi wa utambulisho na kujifanya mtu mwingine

Kifungu cha 31 – Ukwamishaji wa meseji za kielektroniki au uhamishaji wa fedha

Kifungu cha 32 – Uelekezaji wa makusudi wa meseji za kielektroniki sehemu isiyotakiwa

Kifungu cha 33 – Ugaidi unaotokana na makosa ya mtandao

Kifungu cha 34 – Ushawishi wa kusafirisha meseji za kielektroniki Kifungu cha 35- Kuzuia kwa makusudi meseji zilizotumwa kimakosa

Kifungu cha 36 – Kuharibu makusudi meseji za kielektroniki

Kifungu cha 37- Usambazaji haramu wa taswira chafu.

Kifungu cha 38- Matumizi haramu ya habari za kielektroniki

Kifungu cha 39- Kutoa maelekezo ya uwongo

Kifungu cha 40- Kuripoti tishio la mtandaoni

Kifungu cha 41- Mamlaka ya mwajiri kutoa fursa ya kufikia vifaa vya “condes”

Kifungu cha 48 – Kutafuta na kukamata habari zilizohifadhiwa za kompyuta

Kifungu cha 49 – Kurekodi na kuzipata habari

Kifungu cha 50 – Amri ya kuzitoa

Kifungu cha 51- Uhifadhi wa haraka na kufichua sehemu ya habari husika

Kifungu cha 52 – Muda halisi wa ukusanyaji wa habari

Kifungu cha 53- Ukwamishaji wa habari husika Nchi nyingine za Afrika Mashariki zimepitisha sheria ambazo wanaharakati wanalalamika kwamba zinapunguza uhuru wa kujieleza.

Serikali ya Tanzania ilishinda mahakamani kesi moja hivi karibuni dhidi ya wapinzani wa kanuni mpya zinazowataka wamiliki mitandao na wanaharakati kulipia leseni inayofikia hadi Dola 900 (kiasi cha Sh. 2m) na kuwaweka wazi watu wanaowafadhili kifedha.

WAWEZA SOMA:  Zuckerberg achapisha ukurasa mzima kwenye gazeti kuomba radhi juu ya kashfa ya Cambridge Analytica

Mnamo Aprili mwaka huu, Uganda ilitangaza mipango ya kuwatoza kodi watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa