Muongozo: Vitu vya kuzingatia unapotaka kununua simu iliyotumika

Kila mtu anatamani kumiliki simu kali na kisasa, au toleo jipya. Lakini mara nyingi tunashindwa kufikia malengo kwani tunajikuta bajeti mfukoni haikubali kuchukua simu kali. Kwa wastani simu ambayo ni flagship karibia kampuni zote uwa inakuwaga inachezea kwenye shilingi milioni moja kupanda juu,

Mbadala wa kununua simu mpya ni kununua simu iliyotumika. Changamoto kubwa inayokuja kwa kununua simu iliyotumika ni uhakika wa bidhaa unayonunua vs bei utakayolipia, sio hivyo tu hakuna garantii iyo simu itakuwa nzima kwa muda gani tofauti na simu mpya ambazo mara nyingi bei zake zinakuwa zinafanana na hata una uhakika api pa kuanzia ikitokea hitilafu yoyote upoanza kuitumia simu yako.
Kuna aina mbili ya simu zilizotumika kuna aina ya kwanza ambayo ni zile simu zinazorudishwa kiwandani au kwa dealers kutokana na hitilafu ndogo ndogo baada ya kufanyiwa marekebisho haziuzwi ten akama mpya bali kama refurbished. Aina ya pili ni zile simu ambazo zinakuwa zimetumika, mtu kanunua simu yake kaitumia kwa muda fulani na sasa kaamua kuiuza.

Nshawahi kununua simu kadhaa zilizotumika na hazikuwahi kunisumbua

Unaposikia neno “Simu iliyotumika” kitu cha kwanza kinachokuijia kichwani ni “itakuwa ni simu mbovu” au “imemshinda kuitumia anataka amsukumie mtu”. Inawezekana kuna ukweli ila sio lazima iwe hivyo kila wakati. Nshawahi kununua simu kadhaa zilizotumika na hazikuwahi kunisumbua.

Usipokuwa makini mara nyingi unaweza kuuziwa simu mbovu au yenye hitilafu kubwa ambayo gharama za matengenezo zinaweza kutosha kununua simu ingine. Sikatai nshawahi kukutana na bidhaa za namna hiyo pia. Sema kwa sababu najua najua kuhusu simu nagundua mapema na kupotezea.

Leo nimeamua kuandika miongozo hii angalau isaidie katika mchakato wa manunuzi ya simu zilizotumika, mchakato huu unaweza kufaa kuzingatia hata kwa bidhaa zingine kama tableti na kadhalika. Bila kupoteza muda tuanze kuangalia kipengele kimoja baada ya kingine.

1. Jua unataka kununua nini

Sio lazima ujue ni simu ya aina gani specifically, ila anza kupata picha ya simu unayotaka kuinunua kabla hujainunua.

Anza kwa kuchanganua sifa za chini za simu unayoitaka, jua vitu kama RAM, hard disk space, mfumo endeshi ili ujue kama unataka iphone au simu android au simu zenye mifumo endeshi mingine. ukubwa na aina ya kioo, na kitu cha msingi sana ni bajeti yako, lazima ujue utatenga kiasi gani cha fedha kwa ajili ya simu unayotaka kuinunua. Mpaka hapo tunaweza sasa kuanza kupunguza simu ambazo hazitaingia kwenye vigezo vyetu.

Ili ujue utalipia gharama kiasi gani inabidi kwanza ufanye utafiti kidogo

Ili ujue utalipia gharama kiasi gani inabidi kwanza ufanye utafiti kidogo, ulizia bei ya simu mpya kama unayotaka angalau sehemu kadhaa, pitia pitia kwenye mitandao uone bei za simu zilizotumika, kuanzia hapo unaweza kujua sasa unahitaji kuwa na angalau kiasi gani ili upate unachotaka, usiishie hapo. 

Lazima pia ujue vitu vya kuzingatia kuhusiana na hali ya simu ambayo ungependa simu iyo, mfano imetumika kiasi gani? kioo kina michubuko? imewahi kudondoka? ilishawahi kupelekwa kwa fundi ikafunguliwa? Jiridhishe vitu unavovitaka iwe navyo ambavyo unadhani vitakuwa na thamani sawa na fedha yako.

Usikose Kusoma:  Samsung Max: Programu mpya ya Android ya usimamizi na ufuatiliaji wa matumizi ya data.

Kitu kingine ni kufanya timing, kama unataka kununua iPhone 7 basi tulia litoke toleo jipya la iPhone 8, obvious bei ya iPhone 7 itaporomoka kwani watu watakuwa wanauza simu zao za zamani wanunue toleo jipya au madukani wauzaji watashusha bei kwa sababu wanunuaji hawahangaiki sana na toleo lililopita.

2. Sehemu za kununua simu zilizotumika

a) Mtu mnaefahamiana

  • Sehemu ya kwanza kabisa ambayo unaweza kununua simu ni kutoka mtu mnaefahamiana, rafiki yako, ndugu yako, mfanyakazi mwenzako au mtu yeyote ambae mna mawasiliano ya mara kwa mara. Ongea na ndugu zako au watu wako wa karibu kuhusu nia yako ya kununua simu waelezee kama wanaweza kufahamu mtu ambae anauza simu. Cha msingi hapa unakuwa na amani kuwa utakachokinunua hautapigwa na watoto wa mjini. Njia hii ni salama zaidi kwa sababu ikitokea tatizo lolote katikati ya biashara yenu basi mnaweza kutatua pamoja na kwa urahisi zaidi.

b) Mitandao ya kijamii

Siku hizi kwenye mitandao ya kijamii utapata karibu kila kitu unachotaka kuanzia nguo, viatu, vifaa vya kielektroniki na kadhalika. Jaribu kupitia akaunti kadhaa za wauza simu instagram, pitia kwenye ma group facebook na hata whatsapp, wapo wengi tu na wanashindana. Pia kuna mitandao inayojihusisha na kuuza na kununua vitu kama Kupatana, Jumia, Zoom Tanzania na mingine mingi, pitia utakutana na wauzaji wengi. Pia unaweza tembelea mitandao kama jamiiforums kuna watu wengi wanaouza simu.

Vitu vya kuzingatia…

  • Kuwa makini kuna matapeli kibao mtandaoni. Jaribu kupitia review za watu wengine wanasemaje kuhusu muuzaji uyo, hii inaweza kukuepusha na maumivu ya kulizwa na wajanja wa town.
  • Ukifanya kosa mtandaoni na vijana wa mjini “wakakupiga” basi ulie tu. Maana hapo hakuna namna.
  • Usikubali kutumiwa simu, kutana na muuzaji, itest, weka sim card yako, ikiwezekana ambatana na mtaalamu ili akusaidie kukagua mpaka mtakaporidhika ndio mlipie. Toafuti na hapo usinunue.

3. Kukutana na muuzaji

Kuonana na muuzaji ni jambo moja la maana sana, ili upate kuiona simu unayonunua, usiridhike na picha wanazowekaga tu mtandaoni nyingi uwa wanachukua google. Kabla hujapanga kuonana na muuzaji zingatia yafuatayo;

  • Kabla hujaonana na muuzaji, mtaarifu ungependa kuonana nae uitest iyo simu kwa kutumia laini yako, uikague kama inaingiza chaji freshi na vitu vingine. Kama muuzaji hataki kukutana ili uijaribu nadhani ni muda wa kuchanganya na zako utafute muuzaje mwingine.
  • Hakikisha mnakutana na muuzaji kwenye eneo la wazi, sio vichochoroni, unaweza kukabwa na inapendeza kama itakuwa mchana, tena kama utaweza kuambatana na mtu wa ziada inapendeza zaidi kwa sababu za kiusalama,
Usikose Kusoma:  Simu pekee kwa ajili ya makundi maalum katika jamii

4. Ikague simu

Hapa ni kama unanunua mkono kwa mkono na sio muuzaji anakutumia (kama uko mkoani). Kukagua kutasaidia kugundua vitu ambavyo havikuweza kuonekana kwenye tangazo lake, pia unaweza kugundua matatizo madogo madogo ambayo hakuyataja kabla na ambayo unaweza kuyatumia kwa faida yako wakati wa malipo. Na kama muuzaji ni muaminifu atakwambia matatizo yote ya simu hiyo na mnaweza kubaliana pamoja namna ya kuwekana sawa.

unaweza kubeba vitu vifuatavyo wakati unaenda kuikagua:

  • Chaja au waya wa kuchajia
  • microSD card kama simu inakubali kuweka memory card
  • Headphone
  • Laini ya simu ya mtandao unaotumia kwa ajili ya kuitestia

Angalia kama button zinafanya kazi (kama ina button) zibonyeze, Angalia kamera mbele na nyuma kama zina mikwaruzo au michubuko au kama zimepasuka.

Mwisho kabisa, Iwashe simu, angalia kama haina shida yoyote.

5. Kamilisha dili na chukua mzigo

Kabla hujaanza kubishana bei hakikisha umeandaa kiasi ambacho una uhakika hakitazidi hapo na hii ni baada ya kufanya utafiti kule kwenye hatua za mwanzoni. Msikilize muuzaji dau lake analotaka, angalia kama liko chini ya bajeti yako au liko juu, kama liko juu mnaweza anza kubishana point zako zikiwa vitu kama michubuko, na vitu vingine utavoviona wakati wakati unaikagua. ukiona amefika bei unaweza kukamilisha dili na kuchukua mzigo.

Lakini kama muuzaji kakomaa hataki kushuka chini ili afikie bajeti yako na hakuna namna anaweza badili mawazo basi mpotezee na angalia dili lingine. Nna uhakika huwezi kukosa tena baada ya muda mchache tu. Kununua simu haraka haraka au kununua kwa sababu unaihitaji sana kunaweza pelekea upigwe bei au uuziwe kitu kisicho na ubora.

kama muuzaji kakomaa hataki kushuka chini ili afikie bajeti yako na hakuna namna anaweza badili mawazo basi mpotezee na angalia dili lingine.

Hitimisho

Ukitulia ukafanya ukaguzi wako na ukasimamia kwenye kitu unachokitaka unaweza kitu kizuri kwa bei inayoridhisha.

Hata hivyo kununua simu iliyotumika hakuna garantii sana japo hilo lisikuogopeshe sana. Wapo wauzaji waaminifu wa simu zilizotumika na wapo watu kibao wamenunua simu zilizotumika na hawakupata matatizo yoyote.

Kuna jambo nimelisahau? Ungependa tuongeze kitu kwenye orodha? Andika kwenye comment section hapo chini na tutafanyia kazi maoni yako

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa