Kama ilivyokuwa kwa Windows XP na Windows 7 Microsoft imetangaza kuacha kutoa Sasisho za usalama (Security Updates) katika mifumo endeshi ya Windows 8 na Windows 8.1. Hii haina maana Windows 8 na 8.1 zimekufa kama ilivyo Windows XP na Windows 7 tu, bado kama watumiaji wanaotumia Windows 8 au 8.1 wataendelea kupata sasisho hizo za usalama mpaka Januari 10, 2023.
Bila shaka, Windows 10 bado ni bora zaidi kuliko Windows 8 na 8.1 katika suala la vipengele, utumiaji, na usalama hivyo kama unataka mfumo bora wa uendeshaji ambao Microsoft Windows inatoa bado ingekuwa nzuri zaidi kutumia Windows 10, hata kama mfumo wako wa uendeshaji wa Windows 8 bado unapata sasisho za usalama.
Je, bado unatumia Windows 8 au 8.1? Tueleze ni kwa nini hujasasisha kwenda Windows 10 katika maoni hapa chini.