Sasa unaweza kutazama Netflix Bure ukiwa Kenya, baada ya Netflix kuzindua huduma zao nchini humo na kuja na kifurushi cha kuangalia bure. kifurushi hiki kitakuwezesha kuona asilimia 25 ya filamu na michezo ya kuigiza yote ambayo inapatikana kwa watumiaji wa kulipia.
Ili uweze kunufaika na ofa hii, lazima uwe mtumiaji mpya wa netflix, na utaweza kupata ofa hii kupitia simu za mkononi tu. unachotakiwa kufanya ni kuingia netflix.com kujaza taarifa zako ili na ni lazima uwe na miaka 18 au zaidi, hakutakuwa na kipengele cha kujaza malipo.
katika chapisho waliloweka kwenye tovuti yao, Netflix wamesema, “kifurushi hiki cha bure kitaanza kupatikana Kenya kuanzia leo na kuendelea kwa majuma kadhaa. ni imani yetu watu wengi watakaojaribu kifurushi hiki wataipenda netflix kiasi cha kutaka kuwa wateja wa kulipia”.
Hii sio mara ya kwanza kwa Netflix kutoa huduma zao bure (au kwa gharama nafuu sana) kwa wateja wake wapya, uwa inafanya hivyo mara kwa mara hasa kwenye masoko mapya na wanayofanyia majaribio, hutoa vipindi vya bure na filamu kwa wateja wapya.
Watumiaji wa kifurushi cha bure cha Netflix watakosa nini?
- Wataweza kuona asilimia 25 tu ya filamu na michezo ya kuigiza inayopatikana netflix
- Lazima wajiunge kwa kutumia simu za android.
- Hawataweza kudownload ili waangalie wakiwa nje ya mtandao.
- Hawataweza kuonesha filamu kutoka kwenye simu kwenda kwenye TV janja.
Je, Netflix wataweza kuongeza wateja wapya wa kulipia?
watafanikiwa kama tu wataweza kurahisisha njia za malipo, waafrika wengi hasa watu wa afrika mashariki hawatumii kadi za kielektroniki za malipo ambayo ndio njia kuu kwa makampuni mengi ya nje, kama wataweza kuunganisha huduma zao na mifumo ya malipo kwa njia ya simu kama ambavyo Spotify walifanya kenya, basi watawapata wateja wengi.
Kwa sasa makampuni mengi ya konesha filamu na michezo ya kuigiza ya kimarekani kama Netflix na Amazon Prime yanazidi kujipenyeza kwenye masoko ya nje ili kuongeza kasi ya ukuaji wake. Ni imani yetu siku za karibuni na sisi Tanzania tutapata fursa ya kufurahia huduma kama hizi.