Nokia 1 yenye Android Oreo (Go edition) yazinduliwa kwenye kongamano la MWC

Tayari kongamano la MWC 2018 limeanza na makampuni yameanza kutangaza bidhaa wanazozindua, na MHD Global wameanza kwa kutangaza Nokia 1, ambayo ni simu ya bajeti ndogo inayotumia Android Oreo Go Edition.

nokia-1-3

Simu hii inatarajiwa kuuzwa kwa dola za kimarekani 85 ambazo ni takribani shilingi laki 2 za kitanzania. Itaanza kuuzwa kuanzia mwezi wa nne 2018. Simu hii inakuja na rangi mbili Nyekundu na bluu iliyokoza.

nokia-1

Muonekano wake kwa nje ni wa kawaida kabisa, Simu hii imetengezwa kwa kava la plastiki na kava la nyuma linalotoka linalokuja kwa rangi mbalimbali.

Ukiacha Nokia 1, pia HMD Global wametangaza simu zingine ikiwemo Nokia 7 Plus, Nokia 8110 4G huku wakithibitisha kuwa Nokia 6 toleo la 2018 itaanza kuuzwa ulaya miezi kadhaa ijayo. Simu ambayo inatarajiwa kuwa gumzo ni Nokia 8 Sirocco ambayo nayo imetangazwa leo.

nokia-1-2

Sifa za Nokia 1

  • kioo chenye upana wa inchi 4.5
  • Kamera yenye 5-megapixel na LED flash
  • kamera ya selfie yenye 2-megapixel
  • Mfumo endeshi ni Android Oreo Go
  • Betri inayotoka yenye 2,150 mAh
  • Sehemu mbili za kuweka laini
  • Uwezo wa kucheza musiki na Redio ya FM
  • Prosesa ni Quadcore 1.1GHz
  • Ujazo wa 8GB  (ambao unaweza kuongzwa kwa memori card ya mpaka 128GB)

Endelea kubaki nasi ili tukupashe taarifa mbalimbali kuhusu kongamano la MWC 2018. Pia kwa kutufuata kwenye mitandao ya kijamii, na usisahau ku subscribe ili uwe wa kwanza kupata Habari, Uchambuzi na Makala mbali mbali za kisayansi na teknolojia. Pia usisahau ku acha maoni yako hapo chini na unaweza kuwasiliana nasi kwa barua pepe [email protected]

WAWEZA SOMA:  Samsung Galaxy S9: kuzinduliwa Februari 25

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa