Nokia 9 PureView yenye kamera tano yazinduliwa kwenye maonesho ya MWC 2019

HMD Global wamezindua simu janja ya hadhi ya juu ya Nokia 9 PureView. Simu imegusa vichwa vya habari kwa kuwa ndio simu janja ya kwanza duniani kuwa na kamera tano upande wa nyuma zote zikiwa na sensa za megapikseli 12.

Kampuni hiyo inayotengeneza simu zenye jina la Nokia imejinadi ikisema  “kila picha inayopigwa na Nokia 9 PureView iko kwenye mfumo wa HDR, na kamera zote tano zinapiga picha kwa pamoja na kisha kuziunganisha ili kupata picha moja yenye megapikseli 12 iliyo na ubora wa kipekee”

Simu hii inalenga wapiga picha na washabiki wa upigaji wa picha zenye ubora mkubwa. Simu inakubali kutoa picha katika mfumo wa RAW, pia inafanya kazi na app kama Adobe Lightroom mahususi kwa ajili ya kuhariri picha zako moja kwa moja kutoka kwenye simu yako.

Nokia-9

Sifa za Kamera

Kamera tatu zinapiga picha zenye rangi moja, huku zilizobaki mbili zinatoa picha za rangi kabla picha zote hazijaunganshwa pamoja.

Kamera hizi zina uwezo wakuondoa chenga chenga kwenye picha hata kama utazoom hii inaleta ubora zaidi kwenye picha.

Software kwa upande wa kamera pia imeboreshwa zaidi ili kuhakikisha uchakataji wa picha unakuwa maridhawa.

Sifa za simu ya Nokia 9 PureView

 

HAKUNA MAONI

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa