Qualcomm: Simu za kwanza kuwa na teknolojia ya 5G zitatoka mwaka 2019

Mwandishi Diana Benedict

Kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni, inaonekana kwamba kampuni za mawasiliano ya simu zina hamu kabisa kutekeleza 5G haraka iwezekanavyo. Mtengenezaji mkubwa wa Chip za Qualcomm hivi karibuni alitangaza kuwa wazalishaji 18 wa Simu za Mkononi watakua na modem yake ya 5G kuanzia mwaka 2019. Orodha hii ni pamoja na Sony, Asus, LG, HTC, Nokia / HMD, Xiaomi, Oppo, Vivo, ZTE, Sharp, Fujitsu, na wengine.

Qualcomm 5g network

Makamu wa raisi wa Qualcomm Technologies, Inc. bwana Alex Katouzian alisikika akisema, Qualcomm Technologies imejidhatiti kusaidia wateja wake (watengenezaji wa simu janja na vifaa vingine) kusambaza teknolojia hii ya kizazi kijacho ya 5G kwa watumiaji wa mwisho, ambapo simu zitahitaji kuwa na modemu ya Snapdragon X50 5G.

Ujio wa teknolojia hii ya 5G utapanua wigo wa utendaji kazi wa vifaa vya mkononi, ambapo kasi ya upakuaji itaongezeka sana kwa watumiaji wa simu za mkononi.

Kwa sasa nchini Tanzania, teknolojia ya 4G inajitahidi kusambaa kwa kasi ya kuridhisha ambapo mpaka sasa si makampuni yote ya simu yanatoa huduma hiyo. Makampuni ya Simu ikiwemo Vodacom Hapa Tanzania zinatamani sana kutekeleza mtandao wa 5G haraka iwezekanavyo. Teknolojia mpya inayoahidi kufikia kasi ya hadi 1Gb/s (Gigabit Moja kwa Sekunde) katika kupakua, na kupunguza uthabiti.

Hata hivyo Apple na Samsung haijaonekana kwenye orodha ya Utekelezaji huu wa Chip za 5G japo Samsung ilitangaza makubaliano hayo ya kuweka chip za 5G.

Tufuatilie kwenye mitandao mbali mbali ili usipitwe na Habari, Uchambuzi naMakala mbali mbali ya mitanadoni na ya kiteknolojia kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Google+ na Youtube, Pia usisite kutoa maoni yako hapo chini au tuandikie barua pepe kwa mhariri@mtaawasaba.com

Avatar of diana benedict
Mwandishi Diana Benedict Mwandishi
Mitandao ya Kijamii
Diana Benedict. Digital Creator | IT Specialist | Graphics Designer | Web Designer | Web SEO | Contents Management | UI/UX Designer and Social Media Management.
Maoni yako

Trending on Mtaawasaba

Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive