Nubia Alpha: Simu janja inayovaliwa mkononi.

Wakati dunia imeweka macho yake kwenye teknolojia mpya ya simu zenye vioom vinavyojikunja, kmapunia ya simu janja ya Nubia imeamua kupitia njia nyingine kwa teknolojia hiyo hiyo ya vioo vinavyojikunja, kwa kuja na muunganiko wa smartwatch-simu.

simu hii iliyopewa jina Nubia Alpha imetangazwa rasmi kwenye maonesho ya Mobile World Congress, kwa kutumia kioo cha OLED kinachojikunja kuja na muundo ambao haukutegemewa siku za hivi karibuni.

Simu/saa janja hii inakuja na kioo cha OLED urefu inchi 4 kutoka kona moja mpaka ingine, na kina resolution ya 960 kwa 192 pikseli, ambacho ni okay vifaa vyenye skrini ndogo.

screenshot_2019-02-26_at_08.48.10

simu hii inaweza kufanya karibu kila kitu ambacho simu zingine zinafanya, inaweza kupiga simu, kutuma sms kwa kutumia keyboard ya T9 na ina kamera, hebu fikiria unapiga picha kutoka mkononi kwako.

Simu hii inakuja na prosesa ya Snapdragon Wear 2100 iliyotoka mwaka 2016. RAM ya GB 1, na hifadhi ya GB 8. Simu hii ina betri yenye uwezo wa 500mAh, kwa mujibu wa mtengenezaji wa simu hii anadai inaweza kukaa na chaji mpaka siku mbili za matumizi ya kawaida.

Simu hii inaweza kukunjwa mpaka mara 100,000 kabla haijaanza kupoteza uwezo wake wa kujikunja, hii ni sawa na muda mwingi wa kutosha tu, kabla teknolojia zingine hazijaja.

screenshot_2019-02-26_at_08.48.18

Simu hii inayovaliwa haina jipya sana zaidi ya teknolojia ya kioo kinachojikunja, tumeshaona saa janja zenye uwezo wa kupiga simu na kazi zingine simu hii inaweza kufanya, ukiachana na muonekano wake wa kipekee hatuna uhakika kama itakuwa ni rahisi kuitumia kwa matumizi ya kila siku. Tusubiri itakapoingia sokoni.

WAWEZA SOMA:  Mahakama Kenya Yazuia Baadhi ya Vifungu vya Sheria ya Makosa ya Mtandaoni

Simu hii kama ilivyo kwa simu zingine zenye vioo vinavyokunjika inakuja na gharama yake, kwa muundo wa simu hii wenye bluetooth pekee itaingia sokoni kwa gharama ya euro 450, wakati kwa toleo lenye eSim kutakuwa na ongezeko la euro 100 zaidi.

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa