Apple waonya: Pikipiki chanzo cha kuharibu simu za iPhone

Alexander Nkwabi Maoni 143
Kama wewe ni mpandaji mzuri wa bodaboda au pikipiki, basi unatakiwa uiweke simu yako ya iPhone mfukoni. Katika chapisho liliwekwa kwenye tovuti ya Apple, Apple waonya kwamba Pikipiki chanzo cha kuharibu simu za iPhone. wameandika kuiweka simu yako karibu na mitikisiko hupunguza ubora wa ufanyaji kazi wa kamera ya iPhone. Apple walisisitiza mitikisiko hiyo ni ile ya injini za pikipiki.

“Mitikisiko ya juu hasa inayotokana na injini kubwa za pikipiki inaweza kushusha ubora wa mfumo wa kamera,”  

Apple watoa ufafanuzi

Kamera za iPhone zinatumia teknolojia kama vile optical image stabilization na closed-loop autofocus ambazo hukinzana na mitikisiko au mwendo ili kutengeneza picha angavu. Lakini sasa mitikisiko mikubwa ya pikipiki inaweza kuathiri ufanyaji kazi wa teknolojia hizi na kuitumia simu muda mwingi kwenye pikipiki husababisha simu kushindwa kutoa picha kali. Apple wameandika.

Kwa mujibu wa Apple, angalizo hili haliwagusi sana watu wanaotumia pikipiki ndogo au pikipiki zinazotumia umeme aina ya “mopeds” na “scooters”.

Mwandishi Alexander Nkwabi Mhariri
Mitandao ya Kijamii
Alex ni mhariri mwandamizi hapa Mtaawasaba.com, kwa kipindi kirefu amekuwa akivutiwa na mfumo endeshi wa Android na michezo ya kompyuta. Alex akiwa haandiki hapa Mtaawasaba basi hupendelea kupiga picha, kusafiri na kusoma vitabu.
Maoni yako
Receive Mtaawasaba notifications Click ‘Receive,’ then ‘Allow’ when prompted. Dismiss Receive