Raia Uganda kutozwa kodi kila watakapotumia mitandao ya kijamii

Bunge la Uganda laidhinisha mswada tata siku ya Jumatano utakaowataka watumiaji wa mitandao ya kijamii kulipia ili kutumia mitandao hiyo. Chini ya sheria hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kutekelezwa 1 Julai, wanaotumia mitandao ya kijamii watakuwa wanatozwa shilingi 200 za Uganda ambazo ni sawa na ( TSH 120) kila siku.

Hata hivyo wabunge watatu wameonekana kukosoa sheria hizi mpya kwa kuzitaja kama “utozaji wa kodi kupita kiasi “, kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor.

Mbunge wa jimbo Kyaddondo Mashariki Robert Kyaggulanyi, almaarufu Bobi Wine – pamoja na wenzake Joshua Anywarach na Silas Aogon – wamesema kwa sababu watumiaji wa mtandao wa WhatsApp hupata huduma hiyo kupitia muda salio ambalo wanalipia ushuru, ushuru wa ziada utakuwa unakiuka haki.

Raisi Yoweri Museveni alipendekeza kuwepo na ushuru kwenye muda wa maongezi, mawasiliano ya sauti na mawasiliano yasiyo ya elimu(kama matumizi ya mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Whatsapp na wengine.), hii ilikuja baada ya kuona vyombo vya ukusanyaji kodi vinalega lega.

 

 

WAWEZA SOMA:  Sasa unaweza kufanya manunuzi Google Play kwa kutumia M-Pesa (Kenya)

Andika Maoni

Andika maoni yako
Andika jina lako hapa